Familia ya Msuya na Mtengeti wanasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wao Kanali (mstaafu) Ahmed Aboubakar Msuya kilicho tokea jana alfajiri tarehe 7/4/19. 

Marehemu Kanali Msuya ni miongoni mwa kizazi cha vijana  wa Taifa huru la Tanzania waliojiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakati wa harakati za ukombozi wa kusini mwa Afrika. 

Alilijunga na Jeshi la Wananchi kutokana na ushawishi na hamasa alizozipata kutoka kwa Meja Jenerali Sarakikya alipotembelea shule ni kwao. 

Kama vijana wengi wazalendo wa rika lake miaka hiyo, kijana Ahmed alishikwa na hamasa ya kulitumikia Taifa lake na kulikomboa bara la Afrika kutoka kwa wakoloni na ma beberu.  

Baada ya kujiandikisha na kujiunga na JWTZ. Ahmed Msuya alipata mafunzo ya awali ya kijeshi katika chuo cha maofisa wa jeshi Monduli. kati ya vijana walio kuwepo Monduli wakati huo ni pamoja na Rais mstaafu Mh Kikwete.
 Baadae alipelekwa Canada aliposomea Uhandisi. 

Msuya alipigana Namibia na Kagera. Mnamo mwaka 1981 alialikwa Ikulu DSM  na amiri jeshi mkuu wa wakati huo Hayati Mwalimu Nyerere kwa chakula cha mchana. Baada ya maongezi na chakula, Mwalimu alimtishwa askari kijana na mahiri Ahmed Msuya jukumu la kutafuta eneo sahihi na muafaka kwa ujenzi wa kambi ya uchunguzi na Maendeleo ya Uhandisi wakijeshi iliyokuja ikijulikana kama NYUMBU.  

Wakati huo alikuwa na cheo cha Kapteni. Kapteni Msuya alikabidhiwa helicopter na kuzunguka maeneo ya Pwani. Alivutiwa na eneo aliloliona Kibaha ambalo aliliona ni bora kimkakati, kimsingi na kiusalama. Haraka sana aliwataarifu makanda wake wakuu, ambao nao walikubaliana na chaguo lake bila ubishi na ujenzi wa kambi ya Nyumbu ukaanza. 

 Kapteni Msuya alikutana na Balozi Msuya,  mkewe wa miaka 35 mwaka 1982/83 London England na walioana mwaka 1983. Kanali Msuya alitumikia jeshi la Wananchi katika kambi ya Nyumbu na alishiriki katika kubuni na kuzalisha  mfano (prototypes) mbali mbali za magari ya kijeshi na kiraia. 

Alifanya kazi na warika lake pale nyumbu kama kina Kanali Ngingite na Brigadier Simbakalia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...