Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki Zawadi Mbwambo aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo akiwa ameshika mche wa mti kabla ya kuupanda katika eneo la Kilongawima lililopo Kunduchi jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya kilele cha upandaji miti kitaifa. 
 Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki Zawadi Mbwambo kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) akipanda mti katika eneo la Kilongawima jijini Dar es Salaam jana  Aprili 1,2019 ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya siku ya upandaji miti kitaifa nchini.

 Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki Zawadi Mbwambo kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) akizungumza jana jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya upandaji miti kitaifa nchini ambapo ametumia nafasi hiyo kuhamasisha watanzania kupanda miti kwa wingi.
 Mkurugenzi wa Miradi wa Great Hope Foundation Noella Mahuvi  akipanda mti katika eneo la Kilongawimba lililoko Kunduchi jijini Dar es Salaam.

 Mmoja ya wakazi wa wa Kilongawimba akishiriki upandaji miti katika eneo hilo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya upandaji miti kitaifa ambayo yamefanyika leo Aprili Mosi mwaka huu.

 Baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) wakishiriki upandaji miti katika eneo la Kilongawima jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa waandishi wa habari kutoka Michuzi Blog na Michuzi TV Said Mwishehe akipanda mti katika eneo la Kilongawima ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa nchini.







Said Mwishehe,Globu ya jamii 

WAKATI leo ikiwa ni Siku ya Maadhimisho ya kilele cha Upandaji Miti nchini kitaifa,Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umesema kuna kila sababu kwa Watanzania kuendelea kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu ili kukabiliana na kasi ya uharibifu wa mazingira inayoendelea kufanywa na baadhi ya watu. 

TFS katika kuhakikisha miti inaendelea kupandwa leo wameadhimisha siku hiyo kwa kupanda miti katika mikoa mbalimbali ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam ambapo wamepanda miti zaidi ya 1000. 

Akizungumza wakati wa upandaji miti katika eneo la Kilongawima lililoko Kunduchi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki Zawadi Mbwambo aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo amesema ni jukumu la kila Mtanzania kupanda miti iwe ya mbao, matunda au kivuli kwani kwa kufanya hivyo kutasaia uwepo wa misitu ambayo faida zake ni nyingi ikiwemo ya kuzalisha hewa safi kwa ajili ya binadamu. 

Amesisitiza kuwa ni kilele cha maadhimisho ya upandaji miti, hivyo TFS imeendelea na utaratibu wake wa kupanda miti katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba kwa mwaka huu wameamua kuweka utaratibu kila mkoa kupanda miti na wanaendelea kuhamasisha jamii ya watanzania kuwa na utamaduni wa kupanda miti kila siku na isiwe mara moja tu kwa mwaka. 

"Kupanda miti iwe ni jambo la kila siku bila kujali unapanda miti kiasi gani.Nitoe mfano hapa hapa Dar es Salaam kuna watu hawalali kwasababu ya joto ambalo msingi wake unatokana na kukosekana kwa miti kwenye maeneo hayo wakati kuna maeneo mengine ya Dar hakuna joto kwasababu tu wananchi wa maeneo hayo wamepanda miti kwa wingi na kufanya hali ya hewa kuwa tulivu na hakuna joto.Hivyo tunaendelea kuhamasisha watu kupanda miti kadri wanavyoweza. 

"Pia tunahimiza upandaji miti kwasababu itasaidia kuondoa athari 

mbalimbali zikiwemo za hewa ya ukaa.TFS pamoja na kuhimiza Watanzania kupanda miti tumebaliana kila mkoa upande miti.Tunafahamu kasi ya uharibifu misitu ni kubwa mno kulikoa kupanda, hivyo tunaendelea kupanda miti alau kuddhibiti uharibifu wa misitu na ukataji miti hovyo.Kwetu tunaamini upandaji huu wa miti malengo yake ni mawili moja kurudisha misitu ya asili na pili kukabiliana na uharibifu wa ukataji miti kwa kupanda miti,"amesema. 

Ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa waandishi wa habari nao kujenga utamaduni wa kupanda miti mbali ya kuhamasisha upandaji miti nchini kwani kwa kufanya hivyo nao watakuwa sahemu ya watanzania ambao wamepanda miti kwa maslahi ya nchi yetu na uhai wa misitu nchini. 

Kuhusu miti ambayo imepandwa Kilongawima amesema katika eneo hilo TFS imepanda miti 1000 ikiwemo ya mikoko ambayo moja ya kazi yake kubwa ni kulinda mmomonyo wa ardhi, inazuia mafuriko katika maeneo ya ukanda wa Pwani, pamoja kubadilisha hewa ukaa. 

Kwa upande wake Meneja wa Misiti wa TFS Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Dotto Tumbikwa amesema baada ya kupanda miti hiyo ni jukumu lao kuhakisha inalindwa, hivyo ametoa rai kwa wananchi kuhakiksha wanakuwa walinzi wa miti hiyo. 

"Miti ambayo imepandwa leo ni wajibu wetu TFS kuilinda , tutaendelea kushirikiana na wananchi wa maeneo haya kuwahakikisha tunasaidiana nao kuilinda.Tunafahamu faida za uwepo wa miti katika maeno yetu,"amesma na kuongeza kuwa wanaendelea kutoa mwito kwa Watanzania kote nchini kujenga tabia ya kupanda miti. 

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Miradi wa Great Hope Foundation Noella Mahuvi amesema wanatambua umuhimu wa misitu, hivyo wameona ni vema akaungana na TFS katika kupanda miti eneo hilo huku akitumia nafasi hiyo kueleza kuwa umedika wakati kwa wanafunzi katika shule mbalimbali nchini kupanda miti. 

"Ni wajibu wetu kuendeleza uwepo wa misitu nchini, na hii itatokana kwa sisi wenyewe kuamua kuilinda misitu iliyopo, kuzuia uharibifu wa misitu na kubwa zaidi kuendelea kupanda miti .Hivyo nitoe rai kwa wanafunzi nchini kushiriki kikamilifu katika kupanda miti,"amesema Mahuvi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...