Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KITUO cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kimemshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa namna anavyokipigania kituo hicho kufanikisha majukumu yake huku kikitoa rai kwa taasisi nyingine nchini kuacha kufungia viwanda na biashara kwani madhara yake ni makubwa.

Akizungumza leo Aprili 25,2019 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Geoffrey Mwambe amesema wanamshukuru Rais kwani anawapigania sana akiwa katika ziara yake ya Lindi,Mtwara,Ruvuma na Njombe ametoa maagizo na maelekezo kwa TIC na taasisi nyingine zinazohusika na uwekezaji.

"Huu ni wakati wa kuacha kufikiria misaada na badala yake ni kuweka mipango kufanya uwekezaji, Rais anataka rasilimali zetu zitumike kuleta maendeleo. Kwa rasilimali ambazo nchi yetu inazo ni matajiri,nchi nyingine wanamiliki milima na barafu tu.  

"Kwetu sisi TIC Rais anatusaidia sana na imefika mahali akasema iwapo TIC haipewi nguvu kama yeye anavyotaka yupo tayari kituo cha uwekezaji kihamie katika ofisi yake lakini Waziri Mkuu naye amesema hayuko tayari kuona inaondoka kwake,"amesema.

Amefafanua pamoja na mafanikio ambayo yamepatikana TIC bado shida iko katika upatikaji huduma kwa wawekezaji na hiyo haiko kwao na tayari Waziri Mkuu amesema yupo tayari kukaa na wadau wengine kuweka mikakati itakayofaniksha wote kuzungumza lugha moja ya uwekezaji.

Mwambe amesema kila taasisi ijitoe kwa ajili ya maendeleo ya nchi na hivyo wanatoa ahadi kwa Rais kuwa wataendelea kupambana na kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili dhamira njema ya Serikali ya Awamu ya Tano iweze kutimia katika kufanikisha uwekezaji nchini.

Kuhusu kufungiwa kwa wafanyabiashara na viwanda kwasababu ya kudaiwa kodi au vibali vingine kwa wawekezaji, Mwambe ametoa ushauri badala ya kufungia ni vema hiyo ikawa hatua ya mwisho kabisa kwani madhara yake ni mengi kuliko faida.

 " Ni vema taasisi nyingine zifahamu kufunga biashara za watu na kufunga kiwanda ni kuongeza hasara na iwapo kuna ulazima wa kufunga basi iwe hatua ya mwisho. Hivyo hakuna saabu ya kufunga biashara zipo njia nyingi za kufanya na biashara zikaendelea Unapofunga biashara kwa sababu ya kudai kodi , ukweli hutapata hiyo kodi na hakutakuwa na biashara,"amesema.

Amefafanua yeye ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) na katika vikao vya bodi  wamekuwa wakijadili kuhusu namna bora ya kudai kodi na wamekuwa wakikataa kufungia biashara na akaunti za wafanyabiashara.

"Mkurugenzi Mkuu wa TRA mara kadhaa amekuwa akieleza kufunga akaunti ni mchakato mgumu na sio kazi rahisi  na pale ambapo kutakuwa na kesi maalum kuna taratibu za kuafuatwa,"amesema Mwambe.

Amesisitiza "Kuna wimbi la watumishi wa TRA kwenda kufunga biashara za watu jambo ambalo si sawa. Kuna biashara ambazo kodi wanalipa kila siku,hivyo kufunga biashara maana yake TRA haitapata kodi na deni halitalipwa.Ninaumia sana ninapoona yale ambayo tunayazungumza kwenye bodi hayapo kwa watumishi wengine".

Wakati huo huo amesema ni wakati muafaka kwa kila taasisi kuhakikisha inafanya kazi kwa bidii ili kuondoa malalamiko yanayotolewa na wawekezaji nchini na iwe mwisho kuendelea kusikia malalamiko yakitolewa.

Pia Mwambe amesema Rais Magufuli amekuwa akishangazwa na idadi ndogo ya walipaji kado ambayo ni milioni mbili wakati kuna Watanzania zaidi ya milioni 50, hivyo ni wajibu wao kuhamasisha uwekezaji na hatimaye kuongeza idadi ya walipa kodi.

Mwambe pia amesema wanamshukuru Rais kwa kuwapa Jengo jipya lililopo pembeni mwa Jengo la ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kuwa makao makuu ya TIC na hivyo watahamia katika ofisi hizo siku za karibuni.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Geoffrey Mwambe akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu jitihada za kituo hicho katika kuhamasisha uwekezaji nchini
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)Geoffrey Mwambe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia namna ambavyo Rais Dk.John Magufuli ambavyo amekuwa karibu na kituo hicho ili kitekeleze vema majukumu yake.
 Mkurugenzi Mtendaji was Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC)Geoffrey Mwambe (wa kwanza kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam leo Aprili 25,2019

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...