SUALA la ukuzaji wa kada ya ujasiriamali mdogo na wa kati (SME) siyo tu limesisitizwa na Ilani ya Chama Tawala, bali pia ni utekelezaji wa majukumu ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kama lilivyoanishwa na Mpango Mkakati wa Kituo 2016-2021.

Hivyo katika kutekeleza majukumu hayo Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe, aliyekuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo la uchumi na uwekezaji lililoandaliwa na UVCCM amefafanua mambo mbalimbali kuhusu uwekezaji nchini.

Kongamano hilo limefanyika mkoani Mtwara ambapo kwa sehemu kubwa lilijikita kujadili uwekezaji unavyotatua changamoto za ajira kwa vijana.

Hotuba ya Mwambe kwenye kongamano hilo imewatia hamasa vijana ambapo amewataka kujiamini na kuthubutu katika kuibua na kutekeleza miradi ya uchumi kwenye sekta za kipaumbele ambazo ni kilimo, viwanda, madini, mifugo na uvuvi.

Pia amewaaleza washiriki kutafiti na kutambua fursa zinazowazunguka mahali walipo na kuibua miradi ya uwekezaji inayoweza kutekelezwa kwa lengo la kutengeneza ajira na kuzalisha bidhaa au huduma zinazolenga kuinufaisha jamii na Taifa kwa ujumla.

Amefafanua kuwq kwa muktadha huo vijana amesema kuwamtazamo wao wa kwanza wa kupata ajira iwe ni ile inayotokana na uwekezaji wao wenyewe/ kujiajiri. Hivyo kujiamini na kuthubutu ni hatua kwa vijana katika kutengeneza ajira badala ya kutegemea dhana iliyozoeleka ya kutafuta ama kusubiri kuajiriwa.

"Elimu ya uwekezaji na uchumi iliyotolewa kupitia kongamno hili, inatafsiriwa kuwa ni mbegu bora ya maendeleo iliyopandwa kwa takribani washiriki 600 wengi wao wakiwa vijana ambao ni wawekezaji watarajiwa kwa jamii ya Watanzania na Taifa kiujumla.

"Kinachotakiwa ni vijana kuanza utekelezaji wa kuyaishi yote waliyoelekezwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha vikundi vya watu watano sambamba na kusajili kampuni. Baada ya kusajili kampuni wafuate hatua inayofuata ya kubuni/kuibua miradi mbalimbali ya uchumi kwa utekelezaji," amesema.

Pia Mwambe alisema ‘utekelezaji wa uanzishaji wa vikundi ni hatua muhimu kwa vijana kutokana na ukweli kwamba itawasaidia kunufaika na vyanzo vya fedha za uwezeshaji kutoka Serikalini na sekta binafsi inayotolewa kupitia kwenye vikundi kwa ajili ya mitaji ya kutekeleza shughuli/miradi ya kiuchumi na uwekezaji .

Ametumia kongamano hilo kuwatambulisha washiriki Ofisi za Kanda ambapo kuna Kanda ya Kusini zinapatikana Mtwara Jengo la Mkuu wa Mkoa, Ofisi za TIC Kanda ya Mashariki zinapatikana Dar es Salama Jengo la TIC Makao Makuu na Ofisi za TIC Kanda ya Kati zinapatikana Dodoma Jengo la Manispaa.

Pia kuna ofisi za TIC Kanda ya Magharibi zinapatikana Kigoma Jengo la Mkuu wa Mkoa, ofisi za TIC Kanda ya Kaskazini zinapatikana Moshi Jengo la Mkuu wa Mkoa, Ofisi za TIC Kanda ya Ziwa zinapatikana Mwanza Barabara ya Kenyatta na ofisi za TIC Kanda ya Nyanda ya Juu Kusini zinapatikana Mbeya Jengo la Benki ya NBC.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Moses Machali alitumia kongamano hilo kutoa ufafanuzi zaidi ya kwamba vijana waamke kutumia fursa za uwekezaji zilizopo ili kuibua miradi ya uchumi na uwekezaji katika maeneo yanayowazunguka.

"Vijana kuweni na tabia ya kujishughulisha kutekeleza miradi ya kiuchumi ikilenga maeneo ya uzalishaji, usambazaji na ulaji. Kwa msisitizo Mhe.Machali alisema ‘Vijana wakati huu ni wa kupambana na kuthubutu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

"Ni wajibu wa vijana kuchukua hatua kwa vitendo katika kuanzisha miradi ambayo itachangia kwenye maeneo matatu makuu ya uchumi ambayo ni uzalishaji, usambazaji na ulaji, "amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...