Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kasulu

BAADHI ya wakulima wa Wilayani Kasulu wameiomba serikali kupunguza bei za pembejeo za kilimo hususani mbolea za kupandia na kukuzia ili waweze kulima kilimo chenye tija.

Wakulima hao wameiomba serikali kupunguza bei ya mbolea ya kupandia kutoka shilingi elf sabini bei ya sasa kwa mfuko wa kilo hamsini hadi elf arobaini pia kwa upande wa mbolea ya kukuzia ambayo kwa sasa bei yake ni shilingi elf arobaini kwa mfuko wa kilo hamsini wameomba ipungue hadi elf ishirini.

Hayo wameyasema jana kwenye mafunzo ya siku moja juu ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima wa Wilaya hiyo na mawakala wanaouza pembejeo ambapo mafunzo hayo yalitolewa kwa udhamini wa kampuni ya GSM sambamba na  uzinduzi wa mbolea yao ya GS Agro.

Said Shaaban ni mmoja wa wakulima waliohudhuria mafunzo hayo alisema kuwa kwasasa bei za pembejeo nyingi zipo juu ambapo wakulima wenye kipato cha chini wanashindwa kumudu gharama hizo za bei na kushindwa kulima kilimo cha kisasa chenye tija.

"Unajua sisi tumezowea kulima kwa mazowea tumekuwa tukitumia mbolea kwenye mazao ya chakula tunayolima ambayo ni mahindi na maharage ambapo hatuwezi kupata mavuno mengi sababu ya kutolima kisasa,Serikali naomba ituangalie sisi wakulima wa chini kwa kupunguza bei za pembejeo za kilimo"alisema

Naye Mwezeshaji wa wakulima Fatuma Bahi kutoka kijiji cha Msambala alisema kuwa changamoto wanayokutana ni upungufu wa maofisa ugani katika vijiji hali inayopelekea kata zaidi hata ya tatu kuhudumiwa na ofisa ugani mmoja.

"Tuletewe maofisa ugani vijijini ili waweze kutupa elimu ya kulima kilimo cha kisasa na chenye tija ili tuweze kufikia malengo yetu na ya Taifa,maana sasa wengi unakuta wanalima kilimo cha mazowea bila ya kuwa na elimu yoyote"alisema

Mhandisi kilimo na umwagiliaji wa Mkoa wa Kigoma Yohana Zephania wakulima wengi hawatumii pembejeo badala yake wanalima kilimo cha mazowea na kujikuta wakipata mavuno machache,lakini wakitumia pembejeo watapata uzalishaji mkubwa.

Mkuu wa kitengo cha mauzo kutoka kampuni ya tanzu ya GS Agro Remi Nindi alisema mbali na kampuni yao kuuza mbolea wamekuwa wakiwatembelea wakulima wao mara kwa mara na kujua changamoto zao.

"Huu ni msimu wa pili tunaenda mbolea yetu ya GS Agro imekuwa ikifanya vizuri kwa shuhuda mbalimbali za wakulima,msimu ujao tutabadilisho muonekano wa rangi ya mfuko tunaoweka mbolea pia tukuwa na mbolea kuanzia kilo tano ili wakulima wote waweze kumudu kuinunua na kulima kilimo chenye tija"alisema.

 Mkuu wa Kitengo cha mauzo kutoka kampuni tanzu.ya GS Agro Remi Nindi akiongea na wakulima na mawakala wa pembejeo Wilayani Kasulu baada ya uzinduzi wa mbolea yao ya GS Agro.

 Mbolea za kupandia na kukuzia GS Agro.kutoka kampuni ya GSM zikiwa kwenye mfuko wa kilo 50 zilizozinduliwa Wilayani Kasulu .

Washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo ya matumizi sahihi ya pembejeo 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...