Na Moshy Kiyungi, Dar es Salaam
Aprili 2, 2019.

Baadhi ya vijana wanaochipukia katika tasnia ya usanii wa muziki, hajali kuwa elimu ni muhimu kwa mafanikio yao. Ili kuthibitisha hili, soma makala hii utafahamu historia ya msanii maarufu humu nchini Vanessa Mdee.

Mdee ni msomi wa Chuo Kikuu mwenye shahada ya Sheria, aliyeweka pembeni shahada yake akaelekeza nguvu kwenye  tasnia ya muziki wa Bongo Flava. Vanessa Mdee maarufu kama ‘Vee Money’ alizaliwa Juni 7,1988 jijini Arusha.

Ni msanii wa muziki  mwenye talanta nyingi zikiwemo za kuandika nyimbo pia ni mjasiriamali. Vanessa amekuwa akifahamu tamaduni mbalimbali baada ya kuwa katika majiji mbalimbali duniani kama vile Arusha, New York, Paris na Nairobi.

Alipata elimu ya sekondari katika shule za kisasa zilizopo jijini Arusha, baadae akaenda kupata elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki, alikochukua Shahada ya Sheria. Baadae Mdee kwa haraka akaanza kujishughulisha na maswala ya ubunifu na sanaa.

Kama walivyofanya wanamuziki wengi duniani kuachana fani walizosomea, Mdee ni miongoni mwao.  
Aliiacha fani yake ya Sheria kamaamua kujikita katika masuala ya muziki iliyomletea mafanikio makubwa.

Ikumbukwe kwamba huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, yupo mwanamuziki ajulikanae kwa majina ya Koffi Olomide, msomi wa Chuo Kikuu mwenye shahada mbili. Aliamua kuziweka kando na kufanya muziki.

Mwanzoni mwa mwaka 2007, Mdee alipata fursa ya ukaguzi kwa MTV VJ Search jijini Dar es Salaam. Baadae, alijiunga na Carol na Kule kuwa mwenyeji wa Coca Cola Chart Express.

Mwaka wa 2008, Mdee aliwahi kufanya maonyesho huko Nigeria, Afrika Kusini, Kenya, Msumbiji, Angola, Uganda, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Pia umaarufu wake unalijulikana nchi za Marekani na Brazil.

Mwaka huo huo wa 2008, Mdee alifanya kazi na Shirika la Staying Alive juu ya mradi wa karibu na moyo wake.

Vanessa alipaswa kutembelea Uwanja wa Fisi jijini Dar es Salaam akiambatana na Balozi maalum wa Alive Foundation Kelly Rowland.

Aidha Mdee ni mtangazaji wa vipindi katika Televisheni na redio mbalimbali.

Anafahamika kama mwanamke wa kwanza kutoka nchini Tanzania kutangaza katika kituo maarufu cha luninga MTV Vj, kuanzia mwaka 2007.

Baadae kutangaza katika shindano la Epic Bongo Star Search na kipindi cha dume katika Channel ya ITV .

Mwaka 2012 Mdee alijiunga na kundi la B’Hits na kushirikishwa na msanii nguli Ay pamoja na msanii Ommy  Dimpoz, katika wimbo.

Akitangazia luninga ya Mtv mwaka 2008, akiwa balozi wa Alive Foundation, aliamua kwenda kutembelea Uwanja wa fisi akiambatana na Balozi Kelly Rowland.

Vanessa Mdee pia alijiunga Malaria No More Kampeni, iliyokuwa na lengo la kutokomeza malaria.

Mwaka 2009 Mdee alitangaza katika maonesho ya Sauti Za Busara International Music Festival, ambayo hufanyika Visiwani Zanzibar.

Aidha  mwaka 2011 alikuwa mtangazaji wa kituo cha radio nchini kijulikanacho kama Choice FM na kufanya iterview na wasanii kibao wakiwemo

K'Naan, Kelly Rowland, Mac Miller, Rick Ross, Ludacris, Miguel, Donald, Naazizi, Xtatic, Stella Mwangi, Camp Mulla, Tay Grin, Teargas, Dr. Sid and many more African and International acts.

Vilevile Vanessa aliwahi kupata tunzo na kushiriki katika kazi na matangazo mbalimbali yakiwemo ya Music Awards, Airtel, Coke Studio, Crown Paints, Music Tours mwaka 2014 na kufanya nyimbo kibao ikiwemo ‘Siri’ ,’Hawajui’ na ‘Closer’.

Baadhi ya nyimbo za msanii Vanessa Mdee ni Wet, Juu, Kisela,Cash Madame, Niroge, Banbino na Nobod but Me. Zingine ni Scratch My Back, Kwangu Njoo, Move, Reekado Banks, Bounce, Pumzi ya Mwisho na Hawajui. Mdee aliachia vibao vingine ‘matata’ vya Come Over Shadee, Unfollow, Don’t  You Know, Never Ever, Tusimame , The Way you Are na Closer.

Wengi yawezekana wasiwe wanafahamu kuwa Vanessa Mdee ana dada yake aitwaye Nancy ‘Namtero’ Mdee aka Tero.

Tero alikuwa mtangazaji maarufu wa kipindi cha Str8 Up cha KTN ya Kenya.

Hata hivyo Tero ameachana na fani hiyo kwa sasa na kuanzisha familia.

Vanessa Mdee kama walivyo binaadamu wengine, yupo kwenye mahusiano na mwanamuziki Mtanzania Juma maarufu kama Jux.

Mwisho.

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba 0713331200, 0767331200, 0736331200 na 0784331200.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...