Diwani wa Kata ya Mshindo Ibrahimu Ngwada akifanya mahojiano na mwandishi wa habari Fredy Mgunda wa kituo cha Radio Nuru FM Iringa ambaye amepata mafunzo kutoka Mradi wa Boresha Habari na kukiri kuwepo kwa kero hiyo inayotokana na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuwa na uhaba wa magari ya kuondolea taka katika mitaa mbalimbali.
Mmoja ya wanafunzi akipita katika kontena la kuhifadhia taka taka lilopo manispaa ya Iringa ambalo wananchi wanalilamikia pia
Diwani wa Kata ya Mshindo Ibrahimu Ngwada akifanya mahojiano na mwandishi wa habari Fredy Mgunda wa kituo cha Radio Nuru FM Iringaambaye amepata mafunzo kutoka Mradi wa Boresha Habari akimuoneshea umbali wanakotoka wananchi kuja kutupa taka kwenye kontena hilo

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

WANANCHI wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa wapo hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na serikali kushindwa kuzoa taka kwa wakati katika makontena ya kuhifadhia taka taka mbalimbali zilizopo katika halmashauri hiyo.

Wakizungumza na blog hii wananchi hao walisema kuwa makontena ya kuhifadhia taka taka yamekuwa ni hatari kubwa hasa kwa watoto ambao wanacheza karibu na mazingira ya maeneo hiyo hali inayopelekea kuhofia kupata magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu

“makontena ya kuhifadhia taka taka haya ya kubebea taka taka yanatuathiri sana kutoka na uchafu ulipo,unakuta wametupa Mbwa waliokufa,taka taka zilizooza ambazo ndio zimekuwa zikisababisha magonjwa ya milipiko,hivyo tunaomba serikali iwe makini na haya makontena ya taka taka” walisema Wananchi

Wananchi hao walisema kuwa uongozi wa halmashauri umekuwa ukiwajibu wananchi kuwa tatizo ni kukosekana kwa mafuta kwenye gari ambazo zimekuwa zikitumika kubebea makontena ya kuhifadhia taka taka jambo ambalo limekuwa likiwakera wananchi kutokana na kauli hiyo.

“Mwandishi ukiwaambia viongozi kuhusu tatizo hili la kujazana kwa taka taka kwenye maeneo haya ni kutokana na uongozi wetu wa halmashuri ya manispaa ya Iringa kusema kuwa hawana mafuta,sasa sisi wananchi tunaoteseka tunakuwa hatuna cha kufanya” walisema Wananchi 

Aidha wananchi hao walisema kuwa maeneo mengi ya kutupa taka taka hizo yanapakana na shule za misingi zilizopo katika halmashauri ya manispaa ya Iringa hivyo inapelekea kuhatarisha afya za wanafunzi wetu ambao bado ni watoto wadogo.

Hiki kipindi cha vua na taka zinatupwa karibu kabisa na maeneo ambayo yanashule zetu za msingi na watoto wetu wanapita katika maeneo hayo na wengine wapenda kucheza katika maeneo hivyo ni hatari sana kwa watoto kupata magonjwa ya mlipuko” walisema Wananchi

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mshindo Ibrahimu Ngwada amekiri kuwepo kwa kero kwani inatokana na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuwa na uhaba wa magari ya kuondolea taka katika mitaa mbalimbali.

“Niwaambie ukweli hata mimi ni mmoja ya waathirika wa taka taka hizi ambapo naona hali hii ikiendelea kuwa hivi basi yawezekana kukalipuka kwa magonjwa ya milipuko kutokana nauchafu ulipo na sio kata hii hata kata zingine hali hii ipo kama hapa” alisema Ngwada

Ngwada alisema kuwa mikakati ni kuhakikisha anaibana halmashauri kuchukua uchafu huo uliopo kwenye makontena ya kuhifadhia taka taka yanatolewa kwa wakati maana hakuna namna nyingine zaidi ya hiyo.
“Sisi hatuna uwezo wa kutoa hapa hizi taka taka kuzipeleka Kihesa Kilolo ambao ndio kuna eneo la kutupa taka taka zote za halmashauri ya mji ,hivyo ni lazima halmashuri iwajibike kwa jukumu la kutoa hizi taka taka kwa wakati ili kuwaondolea kero wananchi wetu” alisema Ngwada

Ngwada aliupongeza Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kwa kuwapa mafunzo waandishi wa habari na kusababisha kuibua kero za wananchi na kucha kuandika habari za viongozi tu.

“Kwa kweli mradi huu umenifurahi maana sijawahi kupata waandishi wengi wakija katika kata yangu na kuibua kero za wananchi kama hivi bari hii ndio mara ya kwanza na naomba waandishi wa radio Nuru fm endeleeni hivi hivi kwa kuwa mtatukumbusha viongozi kuwatumika wananchi vilivyo” alisema Ngwada

Katika mafunzo hayo Mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo aliichagua habari hii kutoka group na moja kuwa ndio habari iliyoandikwa kwa kiwango kinachotakiwa kutokana na mafunzo.

Naye afisa afya wa halmashauri ya manispaa ya iringa christian ndenga amesema kuwa changamamoto inayopelekea takataka kukaa muda mrefu kwenye makontena ya kuhifadhia taka taka ya mitaa ni kutokana na mji kukua pamoja na kuharibika kwa magari ya kuzolea taka.

Changamoto kubwa ni kuharibika kwa magari yetu na magari mengine kwenda kufanyiwa matengenezo ya kawaida hivyo kukosekana kwa gari moja tu kwa siku lazima tutazidiwa tu kutoa taka taka hizo.

Licha ya wananchi kulalamikia kuwepo kwa mrundikano wa taka kwa muda mrefu manispaa ya Iringa hivi karibuni imeshika nafasi ya kwanza kati ya manispaa zote hapa nchini kwa usafi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...