Mkuu wa Mauzo wa Tigo kwa mikoa ya Mbeya na Rukwa Ladislaus Karlo (wa kwanza kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi wa Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo Serikalini (GePG) kwa mkoa wa Mbeya namna mteja anavyoweza kutumia simu yake kufanya malipo. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Malipo ya Biashara kwa Tigo Pesa wa Tigo Dennis Sakia na anayefuatia ni Afisa Uhusiano Msaidizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa mazingira Mbeya, Kadri Makongwa.
Afisa Uhusiano Msaidizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa mazingira Mbeya, Kadri Makongwa (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo Serikalini (GePG) kwa mkoa wa Mbeya. Kulia ni Meneja wa Malipo ya Biashara kwa Tigo Pesa wa Tigo Dennis Sakia na kushoto ni . Mkuu wa Mauzo wa Tigo kwa mikoa ya Mbeya na Rukwa Ladislaus Karlo.
Waandishi wa habari wakimskiliza Mkuu wa Mauzo wa Tigo kwa mikoa ya Mbeya na Rukwa Ladislaus Karlo (wa kwanza kushoto) wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo Serikalini (GePG) jijini Mbeya. Wa kwanza kulia ni . Meneja wa Malipo ya Biashara kwa Tigo Pesa wa Tigo Dennis Sakia na anayefuatia ni Afisa Uhusiano Msaidizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya, Kadri Makongwa,



Fanya malipo ya haraka, urahisi na kwa usalama kwa zaidi ya idara 300 za Serikali, mawakala na mamlaka mbali mbali kupitia Tigo Pesa

Wateja wa Kampuni ya Tigo wa mikoa ya Mbeya na Iringa sasa wanaweza kufanya malipo kutumia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) baada ya kampuni hiyo kuongeza malipo ya Serikalini kwenye App yake ya Tigo Pesa.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya (WSSA) Afisa Uhusiano Msaidizi wa WSSA Mbeya Kadri Makongwa, alisema mfumo wa GePG umerahisisha upatikanaji wa ankara na kufanya malipo kwa wananchi na kuongeza kuwa umeleta faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza ubadhirifu na kuongeza mapato kwa idara mbali mbali na taasisi za Serikali 

“Mfumo wa GePG, pia imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza fursa za biashara kwa kampuni zinazotoa huduma za malipo kama Tigo. Wananchi wanaweza kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka ofisi na mashirika ya Serikali ikiwa ni pamoja na za kutoka (WSSA) 

Malipo pia yanaweza kufanyika kwa njia mbali mbali za kimtandao, na kufurahisi na mahali popote kwa njia ya simu za kiganjani, benki au kwa njia ya mtandao.,” alisema 

“Kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi wengi ni moja kati ya malengo mkakati yetu,” alisema Makongwa 

Kwa upande wake Mkuu wa Mauzo wa Tigo kwa Mbeya na Rukwa Ladislaus Karlo alisema “Zaidi ya wateja milioni 7 wanaotumia huduma yetu ya Tigo Pesa sasa wana uwezo zaidi wa kufanya malipo kwa haraka kwenda kwa taasisi, Wizara na wakala wa Serikali zaidi ya 300 kupitia Tigo Pesa USSD, Tigo Pesa App na QR Code,” 

Baadhi ya taasisi za Serikali ambazo malipo yanaweza kufanywa kwa Tigo Pesa ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka za Miji, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mamlaka ya Misitu (TFS), Wizara ya Utalii, Bodi ya Utalii, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka za Maji katika miji ya Mwanza (MWAUWASA), Tanga (Tanga UWASA), Dar es Salaam (DAWASA), Dodoma (DUWASA), Hospitali mbali mbali kama vile Muhimbili, Mwananyamala na idara nyingine zaidi ya 300. 

Ili kufanya malipo kwa kutumia Tigo Pesa App na QR Code, wateja wa Tigo wanahitaji kupakua App ya Tigo Pesa na kuscan QR code kisha kuingiza namba ya siri ili kufanikisha muamala.

Ili kufanya malipo kwa kutumia menu ya Tigo Pesa, mteja anatakiwa kufuata hatua zifuatazo;. 

1) Kupiga *150*01# kisha kuchagua Lipa Bili
2) Kuchagua namba 5 (Malipo ya Serikali)
3) Kuingiza tarakimu 12 za mamlaka au taasisi anayotaka ipokee malipo 
4) Kuingiza kiasi cha fedha anachotaka kulipa
5) Kuingiza namba ya siri kwa ajili ya kuruhusu malipo

Kwa upande mwingine, wateja wanaweza kutumia App ya Tigo Pesa ambayo inarahisisha ufanyaji wa malipo kwa kiasi kikubwa.

Baada ya kukamilisha malipo, wateja wa Tigo watapokea risiti ya kielektoniki kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi unaothibitisha kuwa muamala umefanyika kikamilifu. Risiti hiyo ya kielektroniki inakubalika kama uthibitisho tosha wa malipo na inaweza kusaidia kurahisisha kufuatilia malipo kwa kuwa ni rahisi kuhifadhi na kuipata pale inapohitajika ukilinganisha na risiti za karatasi ambazo ni rahisi kupotea au kuharibika.

Tigo inawakaribisha wateja wake kuanza kutumia huduma hii ya Malipo ya Kieletroniki Serikalini (GepG) sasa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...