Mabaki ya mwili wa aliyekuwa
kiongozi wa waasi wa Angola, Jonas Savimbi, yatazikwa tena kwenye mji wake wa
Lopitanga mwezi ujao.
Taarifa iliyotolewa jana (Mei 20) na
Waziri wa Nchi hiyo Pedro Sebastiao ilieleza kuwa mazishi hayo yangelifanyika
baada ya vipimo vya vinasaba kuthibitisha kuwa mabaki hayo ni ya Savimbi.
Savimbi, ambaye alipigana dhidi ya serikali
ya Kisoshalisti ya Angola katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 27,
aliuawa Februari 22 mwaka 2002 katika mapambano dhidi ya vikosi vya MPLA.
Kifo chake kilifungua njia ya
kufikiwa makubaliano ya amani ambayo yalimaliza moja kati ya mizozo ya muda
mrefu kabisa Barani Afrika, ambao ulizuka baada ya Angola kupata uhuru wake
kutoka Ureno mwaka 1975.
Savimbi alizikwa siku moja baada ya
kuuawa katika Jimbo la Mashariki la Moxico.Vipimo vya vinasaba vilivyofanyika
katika Maabara za Afrika Kusini, Argentina, Ureno na Angola vilithibitisha kuwa
mabaki hayo ni ya mwili wa Savimbi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...