Na Marco Maduhu - Malunde1 blog Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, ametoa msaada wa vifaa vya shule kwenye kituo cha kulea watoto wenye ulemavu ualbino Buhangija Jumuishi kilichopo manispaa ya Shinyanga, kwa ajili ya kuwapatia hamasa ya kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao.

Mboneko ametoa msaada huo leo Mei 25, 2019 akiongozana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, pamoja na Ofisa Maendeleo ya Jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone, kwa kutoa msaada huo wa vifaa vya shule kwa watoto hao.

Amesema msaada wa vifaa hivyo vya shule ameshirikiana na marafiki zake wa Kikundi Cha Computer Digital Women cha Jijini Dar es salaam, ambapo wameguswa na watoto hao wenye ualbino, na kuamua kuwasaidia vifaa hivyo,ili kutoa hamasa kwao ya kusoma kwa bidii.

“Vifaa hivi vya Shule nimeshirikiana na marafiki zangu wa kikundi cha Computer Digital Women cha jijini Dar es salaam, ambapo wameguswa na ninyi na kuamua kuwasaidia ili msome kwa bidii na kutimiza ndoto zenu,”alisema Mboneko.“Vifaa vya shule ambavyo nitawapatia ni madaftari, Counter Book, kalamu za penseli na wino, vifutio, vichongeo, rula, soksi, nguo za ndani kwa watoto wa kike na wa kiume, pamoja na zawadi zingine kama pipi na biskuti,” aliongeza.

Pia aliwapongeza walezi wa kituo hicho kwa kwahudumia watoto hao vizuri na kuwalea kama watoto wao, huku akiwataka waendelea kuboresha hali ya usafi kituoni hapo ili kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko.Naye mkuu wa kituo cha Polisi Shinyanga Mjini (OCS) Grace Salia, aliwahakikisha ulinzi na usalama watoto hao kwenye kituo hicho, ambapo siku zote wamekuwa wakilindwa na askari.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Buhangija Seleman Kipanya ambaye ndiye mlezi mkuu wa kituo hicho, akizungumza kwa niaba ya watoto hao alimpongeza mkuu huyo wa wilaya kwa kutoa vifaa hivyo vya shule pamoja na marafiki zake, ambavyo vitawasaidia katika masomo yao.

Alitaja jumla ya watoto ambao wanalelewa kwenye kituo hicho kuwa wapo 230, wasiosikia 74,Wasioona 36, pamoja na wenye ualbino 140 ambao ndiyo wengi zaidi, na kutoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitokeza ili kuwatatulia baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwataka watoto wenye ualbino wanaolelewa kwenye kituo cha Buhanghija Jumuishi Shinyanga Mjini wasome kwa bidii ili kutimiza Ndoto zao. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Askari Alphonce Bandya (ASP) kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga (RPC) Richard Abwao, akiwasisitiza watoto hao kupenda sana elimu ambayo ndiyo itakuwa mkombozi wa maisha yao.
Mkuu wa kituo cha Polisi Shinyanga Mjini (OCS) Grace Salia, akiwahakikisha ulinzi na usalama watoto hao wenye ualbino.
Watoto wenye Ualbino wakisikiliza nasaha za viongozi juu ya kusoma kwa bidiii.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone akigawa vifaa vya Shule kwa watoto wenye Ualbino.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akigawa vifaa vya shule kwa watoto wenye Ualbino.
Zoezi la ugawaji wa vifaa vya shule likiendelea kwa watoto hao wenye Ualbino.
Watoto wenye Ualbino wakionyesha vifaa vya Shule ambavyo wamepewa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Watoto wenye Ualbino wakionyesha Soksi kwa ajili ya kuvalia kwenye viatu vya shuleni.
Muonekano wa vifaa vya shule.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwaaga watoto hao wenye Ualbino mara baada ya kumaliza kutoa zawadi ya vifaa vya Shule na kuahidi Serikali itaendelea kuwa nao pamoja katika kuwatatulia changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili.
Mwalimu mkuu wa Shule ya Buhanghija Selemani Kipanya ambaye pia ndiye mlezi mkuu wa watoto hao wenye Ualbino akishukuru kwa msaada huo wa vifaa vya shule ambavyo vitawasaidia watoto hao katika masomo yao.Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...