Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT)Profesa Florence Luoga amewaagiza wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya kazi ikiwa ni pamoja na kusimama katika weledi ili kuepuka malalamiko ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakiikumba kada hiyo.

Ameyasema hayo leo Mei 22,2019 alipokuwa akifungua mkutano wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa mahesabu hapa nchini(NBAA)unaondelea jijini Arusha na kuongeza kwa kufanya hivyo kutaongeza imani ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu kwa jamii na taasisi wanazozihudumia.

"Ni vema wahasibu kote nchini kuhakikisha kuwa malipo yote yanayofanyika yapitie katika taasisi za kifedha,ikiwemo mabenki taasisi hizo ziweze kujiendesha na serikali iweze kujiongezea kipato kwa lengo la kukuza pato la Taifa,"amesema Profesa Luoga.

Ameongeza endapo watafuata utaratibu huo utasaidia kuondokana na changamoto ya malipo hewa pamoja na kukabiliana na tatizo kubwa la uingizwaji na uzagaaji wa fedha haramu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi yaTaifa ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu(NBAA),Pius Maneno amesema lengo la mkutano huo wa siku tatu ni kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu.

Ameongeza katika mkutano huo mada 11 zitawasilishwa na kujadiliwa zikiwemo za fedha,Tehama,uadilifu pamoja na muongozo wa wahasibu na wakaguzi wa mahesabu kuhusu suala zima la fedha haramu ikiwemo kanuni za nidhamu.

"Bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu hapa nchini imeendelea kuwaelimisha wahasibu na wakaguzi wa mahesabu hapa nchini kuhusu kufanya kuzingatia wajibu na weledi pindi watekelezapo majukumumu yao,"amesema.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema bodi yake imetunga muongozo ulioanza kutumika tarehe 1aprili mwaka huu kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kuhakikisha wanakagua mahesabu yao lengo likiwa ni kuongeza kodi na Mei 1 mwaka huu umeanza kutumika muongozo wa fedha hamu na Juni 15 zitaanza kutumika kanuni za uadilifu.

Amesema mkutano huu unashirikisha watu 300 ambao ni wahasibu na wakaguzi wa hesabu za kutoka taasisi na mashirika mbalimbali, maofisa kutoka Benki Kuu(BOT),na benki nyingine,wataalamu wa fedha na taasisi za Bima.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bodi yaTaifa ya wahasibu na wakaguzi wa Mahesabu (NBAA),Pius Maneno akizungumza na Waandishi wa habari hii leo
Baadhi ya washiriki pamoja na viongozi wakiwa katika picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...