Wakandarasi wanaoshinda kandarasi za ujenzi wametakiwa kuacha urasimu na  ubabaishaji  kwenye utekekezaji wa kazi wanazolipwa na Serikali  na miradi yote itakayokosa ubora wa viwango isipokelewe.

Pia imeelezwa kwamba  si busara kwa kampuni za ujenzi  zilizopitishwa chini ya taratibu za kisheria, kushinda zabuni na kulipwa fedha  za umma zishindwe kujenga kwa viwango na kumaliza kwa wakati. 

Msimamo huo umetolewa na Afisa Tarafa Mihambwe Wilayani Tandahimba mkoa wa Mtwara Gavana Emmanuel Shilatu  alipokagua ujenzi miradi ya ofisi, soko na choo  katika kiijiji cha Ngongolo  kata ya Miuta. Alisema Wakandarasi wana wajibu wa kutimiza ahadi kama mikataba yao ilivyoeleza, kujenga majengo kumaliza kwa wakati husika kazi zao bila visingizio vyovyote.

"Tabia za uzembe na ubabaishaji mkubwa wa ujenzi chini ya kiwango na miradi mingine kutokuanza kabisa licha ya Mkandarasi kupewa pesa tangu Septemba 2018 inatakiwa ife.

"Ifike mahali  uzalendo utusute na kuona aibu. Tuheshimu fedha za umma na kusimamia matumizi bora. Hatuwezi kupata maendeleo ikiwa tutaongozwa na uzembe au ubadhirifu. Miradi ambayo itakosa kujengwa kwa viwango isipokelewe." Alisema Gavana Shilatu 

Aidha Gavana huyo alitoa agizo kwa Mkandarasi wa ujenzi huo akimtaka kufika kazini mapema na kuiasa Serikali ya Kijiji pamoja na kamati ya ujenzi kuwa makini katika usimamizi miradi  ya maendeleo.

Katika ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na Mtendaji Kata Miuta, Serikali Kijiji cha Ngongolo pamoja na kamati ya ujenzi Kijiji cha Ngongolo.
 Afisa Tarafa Mihambwe Wilayani Tandahimba mkoa wa Mtwara Gavana Emmanuel Shilatu  akikagua wa ujenzi miradi ya ofisi, soko na choo  katika kiijiji cha Ngongolo  kata ya Miuta. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...