Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imetoa mikopo siyo kuwa na riba yenye Sh milioni 400 kwa vikundi 128 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Akizungumza leo katika hafla ya kukabidhi mikopo hiyo awamu ya pili, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Ng’wilabuzu Ludigija, amesema kwa mwaka 2018/2019 walipanga kutoa mikopo ya Sh milioni 537.1.

Amesema katika awamu ya kwanza zilitolewa Sh milioni 250 kwa vikudi 97 na awamu ya pili zimetolewa Sh milioni 150 kwa vikundi 31.“Kwa kuzingatia sera na maelekezo ya Serikali tumekuwa tukitenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kuyawezesha makundi haya.

“Walionufaika wahakikishe wanarejesha fedha hizi kwa wakati ili kujitengenezea nafasi ya kupata mikopo mingine,” aalisema Ludigija.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, amesema kumekuwa na mabadiliko makubwa ya mapato katika halmashauri hiyo kutoka Sh bilioni 3 hadi kufikia Sh bilioni 6 hatua iliyowezesha kuongezeka kwa vikundi vinavyopatiwa mikopo.

“Tulipotoa awamu ya kwanza ya mikopo hakukuwa na vijana waliojitokeza fedha zote walikabidhiwa kinamama na wenye ulemavu. Je, vijana wenzangu mnakwama wapi?“Vijana ndio nguvu kazi ya Taifa hivyo, changamkieni fursa hizi mjikwamue kiuchumi,” alisema Sara.Kati ya vikundi 128 vikundi 92 ni vya wanawake, 28 vya vijana na vinane vya watu wenye ulemavu.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri akimkabidhi hundi Katibu wa kikundi cha Wateule Group,Johaim Sasila leo katika hafla ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Mkuu Wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri akitoa amekabidhi Vitambulisho vya Matibabu ya Bure kwa wazee Katika awamu hii ya kwanza zaidi ya wazee 1000 ndio wamekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri (katikati) akizungumza na wajasiliamali kwenye hafla ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi mbalimbali leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni,Ng’wilabuzu Ludigija akizungumza na wajasiliamali katika hafla ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi mbalimbali leo jijini Dar es Salaam, ambapo aliwaomba kurejesha mikopo yao kwa wakati.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...