Makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Zakaria Vang’ota akiwa sambamba na kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Francis Maghembe waalisema kuwa kupatikana kwa hati safi katika Halmashauri hiyo kutachochea zaidi kasi ya utendaji kazi ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa
Baadhi ya madiwani na watendaji wa halmasahuri ya Mji wa Mafinga wakifuatilia kwa umakini ripoti ya CAG wakati wa baraza maalum la halmashauri hiyo




NA FREDY MGUNDA,MAFINGA.

HALMASHAURI ya mji wa Mafinga imefanikiwa kupata hati safi kutokana na utendaji bora,usimamizi wa miradi ukusanyaji mapato kwenye vyanzo vyake vya ndani katika kipindi cha mwaka 2018-2019.

Akizungumza kwenye kikao maalumu cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kwa lengo la kusoma rasmi taarifa ya CAG kwa niaba ya mkuu wa mkoa, Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Iringa, Lucas Kambelenje alisema Halmashauri hiyo imeweza kupata hati safi katika kipindi cha mwaka 2018 -2019 kutokana na watendaji wake wakiwemo madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano katika suala zima la kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na kipindi cha nyuma. 
‘’Nawapongeza watendaji wa Halmashauri na madiwani kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na kufanikiwa kupata hati safi, hivyo nawapongeza muongeze kasi zaidi kiutendaji na kamwe msibweteke,’’alisema

Aidha aliwataka kufuata misingi imara itayowawezesha kudhibiti mapato na matumizi ya halmashauri kwa kuondoa mapungufu yaliyojitokeza katika kipindi cha nyuma kama kuchelewa kuwasilisha mahesabu kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG) ,kuchelewa kuwasilisha taarifa za matumizi bila ya kuwa na viambatanishi vya malipo .

‘’Pia epukeni kulipa madeni hewa kwa watumishi ama waliokufa,kuacha kazi ama watumishi watoro sehemu za kazi, kwani kufanya hivyo kutapelekea halmashauri kupata hati chafu.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Zakaria Vang’ota alisema kuwa kupatikana kwa hati safi katika Halmashauri hiyo kutachochea zaidi kasi ya utendaji kazi ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.‘’Ni dhahiri kila diwani atatekeleza majukumu yake ili kuweza kudhibiti mapato na matumizi ya halmashuari ma kuweza kufanya vizuri zaidi,‘’alisema Vang’ota.

Hata hivyo Vang’ota aliwahimiza madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na kuwataka kuwatendea haki wananchi ambao wamewachagua kwa kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi kwa kuwatataulia kero zinazowakabilia.Akizungumzia hoja hizo kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Francis Maghembe alisema kuwa watahakikisha hoja zote zinafanyiwa kazi ili kusijitokeze hoja nyingine au kuongezeka kwa madeni ambayo halmashauri inadaiwa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...