Na Agness Francis, Michuzi Tv. 

AFISA habari wa klabu ya Azam FC   Jaffary Iddy Maganga (pichani) amesema  baada ya kupoteza Mchezo uliopita dhidi ya Simba kwa kutoka  suluhu ya bila kufungana wanakaibiriwa tena na kibarua kizito cha kumenyana na Mtibwa Sugar ambayo ni timu kongwe na yenye uzoefu iliyopo ligi kuu muda mrefu. 


Afisa habari huyo akizungumza leo Jijini Dar es Salaam amesema kuwa Kutokana na matokeo ya mchezo ulioyopita dhidi ya wekundu wa msimbazi Simba uliopigwa katika uwanja wa Uhuru mei 13 mwaka huu Jijini Dar es Salaam kumezuka maneno kutoka kwa baadhi ya mshabiki na  viongozi wa klabu hiyo kuwa azam fc ilicheza kwa kukamia ili simba isiweze  kushinda na kuchukua ubingwa ligi kuu Tanzania bara. 

"Tulikwenda uwanjani kucheza na Simba kama Azam ikiwa tulishafungwa  bao 3-1 raundi ya kwanza  tukakubalina na matokeo, kwahiyo tulipoingia mchezo wa pili tulisoma wapi tulipotea na tusije tukapotea tena" amesema Jaffary. 

Aliongezea kwa kusema kuwa " Tumecheza na kupata suluhu ya bila kufungana hatukufurahia ile suluhu tulipanga kutoka na Alma 3 uwanjani, isipokuwa sasa ile sare Simba waliona azam walienda uwanjani kwa kuwakamia"amesema Msemaji huyo.  

Aidha amewaomba mashabiki wa soka kuacha kwenda uwanjani na matokeo yao mkononi, mchezo wa mpira una matokeo matatu kufungwa, kufanga au suluhu. 

Pia amesema mara nyingi Azam anapocheza na timu kubwa na kongwe  hapa nchini Simba au Yanga na matokeo yakiwa timu hizo zimefungwa na azam  kilamoja hulalamika kuwa wamewabania na kukamiwa. 

"Azam haipo Katika ligi kuu kwa ajili ya kumbeba mtu uwajani, tupo kwa ajili ya kujenga  jina na status ya klabu yetu,na kwa ajili ya kupambana kama Azam "amesema Jaffary.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...