Na Seif Mangwangi,
Arusha
KIWANDA cha A
to Z cha jijini hapa kimeingia mkataba wa bilioni 3.5 wa kuzalisha dawa aina ya
AFLASAFE ya kutibia mazao yanayosababisha sumukuvu inayopatikana kwenye mahindi
na karanga na ambayo imekuwa ikisababisha maradhi ya saratani ya ini.
Mbali ya saratani ya ini, Sumukuvu (AFLATOX),
inaelezwa kusababisha kudumaa
kwa watoto ambao wamekuwa wakinywa uji unaotumia unga unaotengenezwa kwa zao la
mahindi pamoja na karanga kwaajili ya lishe
Mtendaji Mkuu wa A to Z,
Kalpesh Shah na Kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mazao ya
kilimo (IITA) yenye makao yake makuu nchini Nigeria, Dkt Kenton Dashell walisema
dawa hiyo itakuwa ni suluhu ya maradhi ya saratani kwa kuwa yamekuwa
yakisababisha vifo vingi kwa wananchi wa Afrika.
DKT Dashell alisema kila
mwaka maelfu ya waafrika wamekuwa wakipoteza maisha kwa maradhi
yanayosababishwa na sumukuvu na kupoteza nguvu kazi ya mataifa mengi ya Afrika,
hivyo kuzalishwa kwa dawa hiyo kutapunguza vifo na kukuza uchumi wa Afrika.
“ Kati ya kampuni
nyingi zilizotenda kuomba mradi wa kuzalisha dawa hii, ni A to Z pekee ndio
iliyoonekana kuwa na sifa na uwezo wa kuizalisha, kwa hiyo nipende tu
kuwapongeza sana kwa kushinda tendaII H,”alisema.
Kwa upande wake
Mtendaji Mkuu wa A to Z, Kalpesh Shah alisema kampuni yake itatumia Bilioni 3.5
katika mradi huo na kwamba dawa hiyo itakayokuwa
ikijulikana kama Aflasafe TZ01, itaanza kutumika nchini Novemba mwaka huu baada
ya uzalishaji kuanza rasmi.
Alisema kwa miaka mingi
A to Z imekuwa ikifanya utafiti wa kugundua dawa ya kutibu Sumukuvu kupitia
taasisi yake ya utafiti ya ATRC, kwa kuwa sumu hiyo imekuwa ikiwasababishia
wakulima hasara kubwa pamoja na kupoteza soko la mazao yao nje ya nchi, hivyo
kugunduliwa kwa dawa hiyo na wao kupata fursa ya kuizalisha ni jitihada za muda
mrefu za kuokoa vifo na kukuza uchumi wa Tanzania na Afrika.
Mtendaji Mkuu wa A TO Z Kalpesh Shah akitambulisha dawa aina ya
Aflasafe ambayo itatumika kunyunyiziwa kwenye mahindi na karanga
kwaajili ya kuua sumukuvu ambayo imekuwa ikisababisha maradhi ya
saratani ya ini.
Kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mazao ya kilimo (IITA), Dkt Kenton Dashell pamoja na Mtendaji Mkuu wa ATOZ Kalpesh Shah wakibadilishana nyaraka za makubaliano ya kuanza uzalishaji wa sawa aina ya Aflasafe kwaajili ya kuua sumukuvu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...