LIVERPOOL FC watakipiga na TOTTENHAM pale kwenye uwanja wa Estadio Metropolitan tarehe 1 Juni 2019 kwenye fainali ya Champions League.

Wakenya wawili, DIVOCK ORIGI wa LIVERPOOL na VICTOR WANYAMA wa TOTTENHAM wanatarajiwa kushuka dimbani siku hiyo.

JALUO ORIGI baba yake ni JALUO wa Kenya akiitwa MIKE OKOTH ambae pia alikuwa mchezaji hodari hadi kuchezea Harambee stars  na baadae akatimka na kuhamia Ubelgiji. ORIGI alitupia kambani mabao 2 kati ya 4 ya WATAALAM LIVERPOOL FC dhidi ya WACHOVU Barcelona.

JALUO WANYAMA ambaye ni kapteni wa Harambee stars  alitoa msaada mkubwa kwa TOTTENHAM dimba la kati hadi kuifurumusha AJAX.

Kwa kuweza kuingia fainali za Champions Lg, Wajaluo hao wawili  wamefuata nyayo za Mjaluo mwenzao MACDONALD MARIGA aliyeingia fainali akichezea INTER MILAN ya Italy ambayo ilitwaa ndoo ya CL mwaka 2010 ilipokuwa ikifundishwa na JOSE MOURINHO.

It is an all Kenyan affair in the CL Final!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...