Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe amesema yeye na Kada wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rostam Aziz wamekatwa mikia huku akimshauri ajikite katika kujadili masuala ya uchumi wa nchi.

Membe amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waaandishi wa habari ambapo ametumia nafasi hiyo kumjibu Rostam baada ya siku za karibuni kumshambulia.

"Kwanza niseme hivi, napata kigugumizi kumjibu rafiki yangu Rostam , lakini Rostam ni mchumi na nikikutana naye nitamshauri kwamba anafanya vizuri katika jamii ya Watanzania anapozungumzia uchumi.

"Rostam inabidi awe anazungumzia masuala ya nchi na sio kujikita kuzungumza mambo binafsi. Kwa levo yetu tunatakiwa kuzungumzia masuala ya kitaifa. "Kwa kuwa Rostam ni mchumi mzuri sana , tunapaswa kujadili kwanini uchumi wetu uko hapa ulipo.Kwanini wafanyabiashara wadogo na wakubwa wanafunga biashara zao,"amesema Membe.

Amesisitiza kuwa "Rostam ni mchumi, sasa huu ndio ushauri wangu kwake, ajielekeze kwenye uchumi. Rostam wewe ni mwenzetu, sisi tumekatwa mikia, hata ukijitahidi vipi mkia wako ni mfupi". Ameongeza anamshauri wawe wanazungumza vitu ambavyo wakizungumza binadamu wanawaheshimu.

"Asijifanye mtoto mzawa badala ya kukubali Rostam na mimi ni watoto wakambo,"amesema Membe huku akimsisitiza ajikite kwenye masuala ya uchumi.

Inadaiwa kuwa Rostam alitoa kauli ya kumzungumzia Membe kuhusu uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwakani huku akimhusisha na masuala ya kugombea urais.

Mh,Rostam Aziz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...