Muogeleaji nyota nchini, Dennis Mhini ni miongoni mwa waogeleaji saba waliochaguliwa na chama cha mchezo wa kuogelea Tanzania (TSA) kuunda timu ya Taifa itakayo wania taji la michuano ya Dunia iliyopangwa kufanyika nchini, Hungary.
Mhini ambaye kwa sasa anasoma na kuogelea katika shule ya St Felix ya Uingereza, ataungana na waogeleaji wenzake, Delvin Barick wa klabu ya Mwanza na muogeleaji wa kike, Kayla Temba ambaye anatokea klabu ya DSC. 
 Waogeleaji wengine ni Laila Rashid kutoka klabu ya Taliss-IST, Christopher Fitzpatrick (Mwanza), Christian Shirima (DSC) na Khaleed Ladha wa Taliss-IST. 
 Gharama za usafiri, maradhi na mahitaji mengine kwa waogeleaji watatu, Mhini, Delvin na Kayla zitatolewa na Shirikisho la mchezo wa kuogelea duniani (Fina) wakati waogeleaji wanne, Laila, Fitzpatrick , Christian Shirima na Khaleed wanatakiwa kusafirishwa na TSA kwa kushirikiana na wadau. 
 Katibu Mkuu wa TSA, Inviolata Itatiro alisema kuwa Fina imewapa fursa ya kuwakilishwa na waogeleaji wengine kutokana na kuridhishwa na maendeleo ya mchezo wa kuogelea nchini. Inviolata alisema kuwa ni vigumu kuamini hivyo kutokana na changamoto zinazoukabili mchezo, ikiwemo ukosefu wa bwawa la kuogelea la kisasa, lakini bado waogeleaji wa Tanzania wamefanikiwa kufanya vyema katika mashindano ya kimataifa. 
 “Tunahitaji sapoti kutoka kwa wadau, kwani Fina ipotayari kuwasafirisha waogeleaji watatu na kocha wao tu. Hawa waliobaki ni kazi ya TSA na wadau, hata hivyo TSA haina fedha kutokana na kuingia madarakani miezi kadhaa iliyopita,” alisema Inviolata.
 Dennis Mhini akichapa maji
Dennis Mhini akichupa hewani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...