Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wameungana na wenzao duniani kushiriki maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo hufanyika Mei Mosi kila mwaka.

Wafanyakazi wa MNH walianza maandamano katika hospitali hii kuelekea Uwanja wa Uhuru ambako wameungana na wenzao kutoka taasisi mbalimbali jijini Dar es Salaam kuadhimisha siku hii muhimu kwa wafanyakazi nchini na duniani kote.

Katika kuadhimisha siku hii wafanyakazi wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujenga uchumi imara, huku kauli mbiu ikiwa ni, “Utawala bora ni kwa maendeleo ya nchi.” Mgeni rasmi katika maadhimisho haya, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ongezeko la mshahara ni moja ya jambo muhimu kwa wafanyakazi na kwamba linamgusa kila mmoja. Pia, ametaka kuwapo kwa usalama mahala pa kazi ili kuondoa hofu kwa wafanyakazi.

“Naomba suala la usalama na afya katika sehemu ya kazi lizingatiwe, pia nawaomba viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kufuatilia usalama na afya mahala pa kazi, niwaombe viongozi wanipatie taarifa ni kampuni zipi hazipeleki michango ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi. Hili lifuatiliwe ili kuondoa kero kwa wafanyakazi.”

Pia, amewapongeza wafanyakazi mbalimbali kwa utumishi bora kwani wamekuwa wakifanya kazi nzuri licha ya kuwapo kwa changamoto mbalimbali. Makonda pia amewapongeza walimu kwa kazi nzuri wanayofanya na amewaleza Watanzania kwamba walimu wanaowajenga watu hasa wanafunzi kufikia mafanikio mazuri katika maisha.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani ambayo hufanyika Mei Mosi kila mwaka.
 Maandamano yakiendelea jijini Dar es Salaam ambako wafanyakazi mbalimbali wameshiriki leo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambako wameshiriki maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani pamoja na wenzao kutoka taasisi na kampuni mbalimbali jijini Dar es Salaam.
 Maandamano yakiendelea karibu na Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam katika barabara ya Taifa.
 Wafanyakazi wa Muhimbili wakiwa na wenzao kutoka taasisi mbalimbali wakishiriki kwenye maandamano leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...