Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na Mwakili wa UNICEF Tanzania Bi. Maniza Zaman alipokwenda kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Mei 10, 2019 Jijini Dodoma.
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Bi. Maniza Zaman (kulia) akimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde. (katikati) ni Bi. Khadija Othman mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Bi. Maniza Zaman, akimweleza jambo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma. (Kulia) ni Bi. Khadija Othman mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mkuu wa Ushauri na Sera za Kijamii Bw. Paul Van Lifford (kushoto), akieleza jambo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (kulia) kuhusu ushirikiano baina ya UNICEF na Serikali katika utekelezaji wa Sera ya Hifadhi ya Jamii (Social Security Policy).
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akioneshwa picha ya Watoto na Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Bi. Maniza Zaman, mara baada ya mazungumzo yao, Jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akijadili jambo Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Bi. Maniza Zaman, mara baada ya mazungumzo yao, Jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akijadili jambo na Mkuu wa Ushauri na Sera za Kijamii Bw. Paul Van Lifford (kulia), (katikati) ni Mkurugenzi wa Hifadhi ya Jamii Bw. Daud Kaali. PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU) .

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa UNICEF nchini Bi. Maniza Zaman ambaye amemaliza muda wake alipomtembelea Ofisi kwake iliyopo Jijini Dodoma. 


Katika mazungumzo yao, Mhe. Mavunde amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa la UNICEF kwa kushirikiana na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo na kwa kutoa misaada katika sekta mbalimbali nchini.

“UNICEF imekuwa ikishirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu katika masuala mbalimbali yaliyolenga kuboresha na kuimarisha utekelezaji wa Sera ya Hifadhi ya Jamii (Social Security Policy of 2003), kuwapatia mafunzo watumishi katika masuala ya virutubishi na hifadhi ya jamii, pia kuwapatia vitendea kazi kama vile komputa na magari ambayo yanatumika kwenye miradi mbalimbali,” alieleza Mavunde.

Aliongeza kuwa, Serikali imeguswa na jitihada za UNICEF na itaendeleza ushirikiano na shirika hilo katika kutekeleza jukumu la kuhudumia Watoto. Aidha, Naibu Waziri Mavunde alimpongeza Bi. Maniza Zaman kwa kazi nzuri aliyofanya kipindi cha muda wake na kumsihi kuendelea kuwa balozi mzuri wa masuala ya Watoto. “Tutakukumbuka kwa juhudi na ushauri uliokuwa ukitupatia katika masuala ya elimu na haki za Watoto,” alisema Mavunde.

Kwa upande wake, Bi. Maniza Zaman amesema anaishukuru Serikali kwa ushirikiano iliompatia kwa kipindi chote alichokuwa hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...