Mchezaji kandanda wa zamani wa Taifa Stars na Yanga na Pan African Jellah Mtagwa yupo kitandani akiugua kiharusi na anahitaji msaada wa matibabu pamoja na kujikimu kimaisha.
Mtagwa, ambaye hivi sasa amepooza nusu ya mwili wake, anaishi Manzese Friend's Corner  jijini Dar es salaam pamoja na familia yake akiwa hana hili wala lile kutokana na maradhi hayo na ufukara.

Wadau na mashabiki wa mpira wa miguu wameelezea masikitiko yao kwa hali kama hiyo kumkumba aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya Taifa Stars ambaye picha yake iliwekwa kwenye stempu kutokana na mchango wake uliotukuka kwa nchi.

Wengi wanahoji endapo kama Shirika la Posta lilimlipa mchezaji huyo mrabaha wa kuwekwa sura yake mwenye stempu, na kama Shirikisho la Mpira nchini (TFF) wana taarifa zake na kama wanamsaidia kwa chochote.

Hivi tunavoongea umoja wa wachezaji soka wa zamani  (UMSOTA) wameanzisha harambee ya kumsaidia mwenzao huyo kwa kuchangishana ili kumsaidia.

Tayari umoja huo umetoa ombi la msaada kwa wasamaria wema kumsaidia Jellah Mtagwa kwa kutangaza namba yake ya simu
Namba 0755 693 330 kwa yeyote atakayeguswa.


 Baadhi ya wachezaji soka wa zamani wakiwa wamemtembelea Jellah Mtagwa nyumbani kwake Manzese Friend's Corner jijini Dar es salaam kumjulia hali na kumpatia msaada




 Baadhi ya wachezaji soka wa zamani wakiwa wamemtembelea Jellah Mtagwa nyumbani kwake Manzese Friend's Corner jijini Dar es salaam kumjulia hali na kumpatia msaada



 Baadhi ya wachezaji soka wa zamani wakiwa  na wanafamilia baada ya kumtembelea Jellah Mtagwa nyumbani kwake Manzese Friend's Corner jijini Dar es salaam kumjulia hali na kumpatia msaada

Stempu iliyowekwa picha ya Jellah Mtagwa
Jellah Mtagwa akisimulia adha ya maradhi yake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...