Kampuni inayojihusisha na uchakatuaji na uuzaji wa gesi asilia nchini Tanzania,PanAfrican Energy Tanzania Ltd, leo imeingia makubaliano na wilaya ya Kilwa,kufadhili ujenzi wa miradi ya afya itakayo gharimu zaidi ya billion moja za kitanzania.

Mkataba huo wenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia mbili (1.2bilion) umesainiwa kati ya viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa na kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania ambao ni wadau wa maendeleo katika Wilaya ya Kilwa. Utiaji saini huo umeshuhudiwa na Mwanasheria wa kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania Ritha Mohele,na Meneja Uwajibikaji kwa jamii wa kampuni hiyo Andrew Kashangaki na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

PanAfrican Energy Tanzania pia imejitoa kuboresha hali za kimaisha katika wilaya ya Kilwa,Mkoani Lindi. PAET imetengeneza miradi hii ya uwajibikaji kwa jamii ikishirikiana na halmashauri ya  wilaya ya Kilwa na viongozi wake pamoja na wasemaji kutoka kwa wananchi wa Kilwa wenyewe.
Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imesaini mkataba wa ujenzi wa Kituo cha Afya Somanga na upanuzi wa hospitali ya Wilaya Kinyonga.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Ndg. Renatus Mchau ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo uliokuja kwa wakati na kueleza kuwa kwa muda mrefu Wilaya ya kilwa ilikuwa na changamoto katika sekta ya Afya lakini kwa sasa changamoto hizo zinakaribia kuiisha kutokana na halmashauri yake kuweka nguvu katika kuzitatua.

‘ Tangu mwaka 2017 tumepokea zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni mia nane kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI katika mpango wa uboreshaji wa Miundo mbinu ya sekta ya Afya ambapo vituo vinne vya Afya vya Masoko, Tingi, Pande na Nanjilinji, na sasa mchango wa hawa wadau wametuongezea nguvu nyingine katika kuendeleza sekta ya Afya. 

Alisema msaada huo wa PanAfrican Energy Tanzania utaongeza idadi ya vituo vya Afya kutoka vitano vya sasa hadi sita ambapo kati ya hivyo vituo vinne vitakuwa na uwezo wa kufanya upasuaji na kuongeza damu kwa wanawake wajawazito.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mhe.Abuu Mjaka amewashukuru kwa mara nyingine kampuni hiyo kwa msaada huo kwani ni mara ya pili wanatoa msaada mkubwa baada ya ujenzi wa awali wa kituo cha Afya cha Nangurukuru. ‘Nyie sasa tunawatambua rasmi si kama wadau tu bali familia ya Kilwa’’ aliongeza Mhe.Mjaka.

Ujenzi Kituo cha Afya cha Somanga ulianza kwa Mchango wa nguvu za wananchi ambapo mpaka sasa jengo la mapokezi lipo katika hatua ya linta ambapo zaidi ya shilingi milioni sabini kutokana na mchango wa wananchi , halmashauri pamoja mchango binafsi toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli wa shilingi milioni ishirini(20,000,000) aliyoitoa mwaka 2017 akiwa katika ziara mkoani Lindi. Mhe.Rais alitoa msaada huo baada ya kuombwa na wananchi waliomsimamisha katika kata ya Somanga, msaada huo ulikuwa chachu kwa wanachi wa kata hiyo na hivyo wakaanda kuchangia nguvu zao.

Upanuzi huo utahusisha ujenzi wa Jengo la mapokezi,Jengo la wazazi, Upasuaji , chumba cha kuhifadhia maiti na chumba cha kufulia nguo vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya milioni mia nane na thelathini.

Katika hospitali ya Wilaya ya Kinyonga upanuzi utahusisha chumba cha kuhifadhia maiti na Bohari ya dawa thamani ya shilingi milioni mia nne.

Baada ya kukamilika kwa ujenzi Kituo cha Afya cha Somanga, Wilaya ya Kilwa itakuwa na vituo vya Afya sita ambavyo ni Somanga, Tingi, Masoko,Nanjilinji , Pande na Njinjo.
Mwanasheria wa kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania Ritha Mohele na Meneja uwajibikaji kwa jamii wa Kampuni hiyo, Andrew Kashangaki, wakiwapa mkataba uliotiwa saini kwa ajili ya ufadhili wa ujenzi wa miradi ya afya itakayo gharimu zaidi ya billion moja za kitanzania.miradi hiyo sehemu ya kuhifadhia maiti, duka la dawa la wilaya na marekebisho ya hospital ya Somanga kwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kilwa Abuu Mjaka na DED wa halmashauri ya wilaya hiyo Renatus Mchau.
Mwanasheria wa kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania, Ritha Mohele akisaini mkataba kwa niaba ya kampuni hiyo,kwa ajili ya ufadhili wa ujenzi wa miradi ya afya itakayo gharimu zaidi ya billion moja za kitanzania.miradi hiyo sehemu ya kuhifadhia maiti, duka la dawa la wilaya na marekebisho ya hospital ya Somanga.
Baadhi ya mashuhuda walio hudhuria kushuhudia mkataba uliotiwa saini kwa ajili ya ufadhili wa ujenzi wa miradi ya afya itakayo gharimu zaidi ya billion moja za kitanzania.miradi hiyo sehemu ya kuhifadhia maiti, duka la dawa la wilaya na marekebisho ya hospital ya Somanga kwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya kilwa Abuu Mjaka,na DED wa halmashauri ya wilaya hiyo Renatus Mchau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...