Na.Khadija seif,Globu ya jamii

MALKIA wa muziki wa Afro Pop nchini Mwanahawa Abdul  a.k.a Queen Darlin  ameiona nyota ya jaha kupitia muziki wa Diamond kufika mbali kisa  Mwanadada Tanasha.

Darlin amesema Tanasha anafanya muziki, na soko lake amelenga mbali sio Afrika Mashariki tu kutokana na kujuana na watu mbalimbali ambao alikuwa akifanya nao kazi kama video vixen .

"Kuwepo lebo ya wasafi classic baby (WCB) ambayo anasimamia kaka yangu diamond hamaanishi kuwa natoa ngoma nikijisikia au ninavopenda mwenyewe, bali ni kanuni na taratibu ambazo zimewekwa kwa kila msanii kutoa wimbo kwa wakati sahihi kulingana na soko linahitaji kitu gani "

Darlin ambaye amekuwa na muonekano wa kimanjonjo awapo jukwaani,amewashukuru mashabiki wake ambao wameupokea vizuri wimbo wake mpya "muhogo" unaofanya vizuri vituo mbalimbali na kujiongezea wigo wa mashabiki kila kona ndani na nje ya nchi,wakiwemo Wanaume kutokana na taswira inayojengeka kwenye wimbo huo.

"Muhogo ni wimbo ambao ulipita BASATAa na kupewa vibali vyote kutokana na wimbo huo kutumia tafisida na kuficha maana halisi, na ndio kitu pekee ambacho hata wimbo wa nyegezi uliotungwa na Rayvan aliomshirikisha Diamond ulifungiwa kutokana na kutokuwepo kwa tafisida kwa baadhi ya matamshi na kuleta ukakasi kwa hadhira, hivyo nilitumia nafasi hiyo katika kutengeneza na kuboresha wimbo wangu,"

Mwanadada huyo ambaye ameonaka kuendelea kutikia anga ya muziki wa Bongofleva kwa upande wa wasanii wa kike,Darlin amebainisha wazi kuwa bado anamkumbuka sana Alikiba katika kushirikiana nae kwenye kazi zake kimuziki na kutengeneza wimbo kama wajua nakupenda uliofanya vizuri miaka ya 2009.

"Alikiba akitoa ngoma mpya naingia Youtube natazama kama nzuri nasifia, kama mbaya naweka wazi sisi ni watu wa karibu sana "

Darlin amewaomba  mashabiki wake waendelee kumuunga mkono kwenye kazi zake na wiki hii anatarajia kutoa ngoma mpya mbili,moja itakayoitwa 'tawire' na 'mbali'aliomshirikisha msanii mwenza wa kundi la WCB .
Mwanahawa Abdul  a.k.a Queen Darlin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...