Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC) itaanza kampeni ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya Ndondo Cup 2019  kesho (Jumanne Mei 14) kwa kupambana na timu ya Rangers.

Mchezo huo umepangwan kufanyika kwenye uwanja wa  Mwalimu Nyerere Mwembe Chai kuanzia saa 10.00 jioni.

Taswa FC ambayo inafanya mazoezi mara moja kwa wiki (Jumamosi)  itakuwa inashiriki kwa mara ya kwanza, ipo katika kundi D pamoja na timu za Ukwamani na Goba Kombaini.

Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa wamejiandaa vyema katika mchezo chini ya makocha wao, Ibrahim Masoud ‘Maestro’ na Saidi Seif.

Majuto alisema kuwa wanajua watapata ushindani mkali kutoka kwa timu ya Rangers, lakini hilo halitazuia kuibuka na ushindi.

Alisema kuwa kila mechi inakuwa na ushindani, lakini si kwa timu za kundi D na kuahidi kufanya vyema katika mechi zao zote.

“Tupo katika mashindano na wapinzani wetu pia wapo katika mashindano. Watashindana, lakini hawatashinda, tupo vizuri katika kila idara na malengo yetu ni kuonyesha kuwa hata waandishi wa habari nao wanaweza kucheza mbali ya kufanya kazi ya kuelimisha jamii,” alisema Majuto.

Alisema kuwa waandaaji wa mashindano ya Ndondo Cup 2019 hawakukosea kuwakubalia kushindana katika mashindano hayo ambayo mpaka sasa yamechangia kiasi kikubwa maendeleo ya soka hapa nchini.

“Nawapongeza waandaji kwa kuwa na mashindano ya soka yenye mvuto wa aina yake na kuhamasisha maendeleo ya soka,

Kuna vijana ambao wametokea katika mashindano haya na sasa wanatesa katika timu za madaraja ya juu, pia kuna wachezaji wamepata fursa ya kufanya majaribio nchi za Ulaya, hii nifaraja kubwa sana kwetu,” alisema.

 Alisema kuwa wanaamini hata Taswa FC itatoa wachezaji ambao watacheza timu kubwa mbali ya kuwa ni wana- habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...