TIMU ya sevilla kuwasili kesho jijini Dar es salaam kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Simba.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Utawala na udhibiti wa kampuni ya sportpesa Abas Tarimba amesema kampuni hiyo inayochezesha michezo ya kubahatisha inaenda kuandika historia kwa mara ya pili kuileta timu ya kimataifa sevilla.

"Mbali na ujio wao timu ya sevilla itaweza kufanya shughuli mbalimbali zenye lengo la kuinua sekta ya michezo nchini kwa vijana "
Tarimba ameeleza kuwa timu hiyo ya kimataifa itapata nafasi ya kutoa  mafunzo kwa timu ya vijana bom bom fc huku kwa baadhi ya maofisa wa klabu ya sevilla wataendesha mafunzo kwa viongozi wa vilabu pamoja na shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) na washiriki wake ili wapate kuhimarika kitaaluma na uelewa jinsi ya kuongeza vipato vya vilabu.

Kwa upande wa msemaji mkuu wa klabu ya wekundu wa msimbazi Haji Manara ameeleza wazi kuwa ujio wao utaleta manufaa makubwa katika sekta ya michezo hasa mpira wa miguu huku taifa likiwa limepata heshima kubwa na Pato la taifa kuongeza.

"Mechi ya sevilla dhidi ya Simba fc itaongeza Pato la taifa kutokana na tayari tiketi zimeshanunuliwa kwa wingi na zinaendelea kununuliwa"

Hata hiyo amesema maandalizi yanaendelea vizuri,kwa sasa timu imeelekea singida kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya singida united hapo kesho .

"Uchovu wa mechi za ligi kuu sio kigezo cha kutokufanya vizuri katika mechi dhidi ya sevilla tutapambana na kuhakikisha tunaitangaza nchi yeti kwa ushindi "

Pia ametoa rai kwa mashabiki wa Simba na timu zingine kujitokeza kuishangilia timu ya Simba ili kwani ndio nafasi pekee ya kwa wachezaji wakitanzania kujitangaza kimataifa kama klabu  na kupata fursa nchi zingine kuwekeza katika sekta ya mpira.
Mkurugenzi wa utawala na udhibiti wa kampuni ya michezo ya kubahatisha nchini (SPORTPESA) Abas Tarimba akizungumza na waandishi wa habari kufatia ujio wa timu ya kimataifa sevilla kutoka nchini Hispania kuwasili kesho kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Simba FC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...