Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha

Ujenzi holela uliojegwa na baadhi ya wananchi  wilaya ya Arumeru imeelezwa kuwa ndio chanzo kikubwa cha mafuriko  yaliotokana na maji kutwaama sehemu moja .

Hayo yamebainishwa na Mkuu Wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro  wakati  
akizungumza na Wananchi Wa Wilaya hiyo waliokumbwa na mafuriko hayo alipofanya 
ziara ya kuwatembelea na kuwapa pole wananchi waliokubwa na mafuriko  
ambayo yamepelekea kuharibiwa kwa baadhi ya Mali zao.

Alisema kuwa ujenzi holela uliojengwa na baadhi ya wananchi ndio 
umesababisha mafuriko hayo ,kwani wananchi baadhi ya wananchi wamejenga  
nyumba katika njia asili zakupitishia maji  .

Aidha aliwataka wananchi wote waliojenga mabondeni  na kuzuia njia asili za  
maji kubomoa Mara moja ili kuepusha mazara makubwa  ambayo yanaweza kutokea  
hapo baadae kama vifo.

 "Mimi nathani hii Mara ya pili hili tatizo kutokea na mwaka Jana lilitokea tena  
mmekaa tumekubaliana  kuvunja kuta zote ambazo zinazuhia maji kupita kwenye  
mkondo wake hivyo basi najua kunawatu wataathirika lakini inabidi ili  
tuweze kutatua tatizo kubwa linaloweza kutokea apo baadae" alisema Muro 

Aliwataka wananchi kufuata sheria za ujenzii  wa miipango miji nakuacha kujenga kiholela holela ilikuondokana na adha inayoweza kuutokea.   

Kwa upande mmoja ya moja ya mwananchi alieathirika Rose Nassari aliishukuru serikali kwa kuwatembelea na kuwapo pole  pamoja na kuwapa elimu ya hasara ya kujenga kwenye mikondo  ya maji.

Mafuriko hayo yamekumba katika baadhi ya kaya za vijiji vya nduruma pamoja na shangarai. picha ikionyesha mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro  akiongea na wananchi wa wilaya  hiyo wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea wananchi wake waliokubwa na tatizo mafuriko  ,ambapo alisema ujenzi hoela  ndio chanzo cha mafuriko hayo na kuwataka wananchi waachie njia za asili za maji  ili yaweze kupita
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na Wananchi wa wilaya hiyo wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea wananchi wake waliokubwa na tatizo mafuriko ,ambapo alisema ujenzi hoela ndio chanzo cha mafuriko hayo na kuwataka wananchi waachie njia za asili za maji ili yaweze kupita

Picha ikionesha mwananchi mmoja wa kijiji cha Shangarahi akiwa
amebebwa mgongoni tayari kwa kuvushwa daraja mara baada ya daraja hilo kusombwa na maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...