Uongozi wa klabu ya Lipuli unapenda kutumia nafasi hii kukanusha vikali ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) unaosambaa katika vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii ukidai Makamu M/Kiti wa klabu hiyo Ayoub Kihwelo amekili kuwa baadhi ya viongozi wa klabu  wamejihusisha na njama za kuihujumu klabu katika michezo yake ya hivi karibuni ikiwemo mchezo dhidi ya Simba SC, Biashara United na Mbeya City. 

Ujumbe huo unadai Ayoub Kihwelo alikiri hayo katika moja ya mohojiano yao na vyombo vya habari ikiwemo redio Ebony Fm ya mkoani Iringa. 

Uongozi unapenda kusema taarifa iliyopo katika ujumbe huo ni uzushi wenye lengo la kuharibu mahusiano ya klabu na wadau wake ikiwemo wanachama na mashabiki wake na kwa muktadha huo uongozi unaomba ujumbe huo upuuzwe.

Uongozi pia unatoa tahadhari kwa wanaoendelea kusambaza ujumbe huo kwani umekwisha wasilisha suala hilo kwa mamlaka husika za makosa ya kimtandao ikiwemo jeshi la Polisi.

Kwa hali hiyo uongozi unaomba radhi kwa wanachama na mashabiki wake kutokana na kuzagaa kwa taarifa hiyo ya uzushi.

Asanteni kwa ushirikiano.

Imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Lipuli, Clement Sanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...