Na Miza Kona Maelezo Zanzibar
Wakala Chakula na Dawa imeanza kujadili muongozo maalum uliotolewa na
Jumuiya ya Afrika Mashariki wenye lengo la kuinusuru jamii na athari
zitakanazo na matumizi ya dawa ambayo hatimae husababisha madhara
mbalimbali kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Afisa kutoka Wakala wa Dawa na Chakula Mohammed
Omar kwenye Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe katika kikao cha wadau
kinachojadili hatua zinazofaa kuepukana na madhara ya dawa na vifaa
tiba.
Amesema lengo la kikao hicho ni kutengeneza Muongozo ambao utawezesha
kufuatilia madhara ya dawa, vifaatiba, tiba asili pamoja na chanjo ili
kupata jamii yenye afya bora na kuepukana na maradhi yanayotokana na
matumizi ya dawa.
Amesema muongozo huo pia utaweza kusaidia kuripoti, kuziwakilisha na
kizitambua kuchunguza na kufuatilia dawa ambazo zinaleta madhara kwa
jamii na kuzitafutia hatua za kuzipatia ufumbuzi kwa kutumia njia
muafaka bila ya kubadilisha dhamira iliyowekwa na Jumuiya hiyo
Amefahamisha kuwa kumekuwa na matatizo makubwa ya madhara ya dawa
ambazo husababisha kupata maradhi yasiyoambukiza kutokana na jamii
kutotumia dawa bila ya kiwango kinachotakiwa.
“Dawa zina faida lakini pia madhara kadri unavyotumia dawa ndio
madhara yanapoonekana hivyo tumeandaa muongozo wa kuweza kuzitambua
dawa zenye kuleta madhara kwa jamii na kuzifanyia kazi kwa kuzifutia
na kuzitambua ili kuweza kuisadia jamii”, alieleza Afisa huyo.
Alisema wameweka fomu kila kituo cha Afya na hospitali kuzitambua dawa
ambazo zinaleta madhara kwa jamii kwa kila mtumiaji ambae atapata
madhara baada ya kutumia ili kupata ufumbuzi na kuisadia muongozo huo
kufanyakazi yake lakini changamoto kubwa iliopo urejeshaji wa fomu
hizo ni mdogo.
Nae MratibuMsaidizi wa Kitengo Shirikishi Ukimwi, Homa ya Ini, Kifua
Kikuu na Ukoma Issa Abeid Mussa amesema muongozo huo utaweza kujadi
namna ya ufuatiliaji wa dawa na kuratibu athari zinazotokana na
madhara utumiaji wa dawa
Ameitaka Wakala wa Dawa na Chakula kuangalia kwa kina na kuzifuatilia
dawa zote zinazoingizwa nchini kabla ya kuzisambaza katika vituo na
kuzitumia ili kuepuka madhara kwa jamii.
MratibuMsaidizi wa Kitengo Shirikishi Ukimwi, Homa ya Ini, Kifua Kikuu na Ukoma Issa Abeid Mussa akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uangalizi wa Dawa zikiwa sokoni katika Mkutano wa siku sita wa kujadili athari zitokanazo na dawa uliofanyika Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
Wadau wa Dawa na Vifaa tiba wakijadili mwangozo
uliotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki wenye lengo la kuhakikisha
matumizi ya dawa na vifaa tiba havileti madhara kwa wananchi katika
Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe.
Picha na Makame Mshenga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...