Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mhe. Kangi Lugola akisisitiza kuhusu agizo lake lakuwataka askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini kuzingatia sharia wanapowachukulia hatua waendesha bodaboda kote nchini leo Bungeni Jijini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. Dkt. Angelina Mabula akieleza mikakati ya Serikali kuimarisha utendaji wa watumishi wa sekta ya ardhi nchini leo Bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Job Ndugai akisisitiza jambo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
  Mbunge wa Mtama mhe Nape Nnauye akisisitiza umuhimu wa kuimarisha sekta ya kilimo hapa nchini hasa mazao ya kimkakati kama korosho leo Bungeni jijini Dodoma wakati wa mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Kilimo.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa Waziri wa habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na Mwanasheria mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi (Katikati) leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanaosoma masomo ya Sayansi ya Siasa wakiwa Bungeni kwa ziara ya mafunzo leo Jijini Dodoma.
Sehemu ya wabunge wakiwasili katika Viwanja vya Bunge leo Jijini Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Bunge unaoendelea Bungeni Jijini Dodoma. (Picha zote na Frank  Mvungi- MAELEZO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...