Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

 AJALI ya kugongana kwa magari miwili ikiwemo gari la  Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) ambapo watu watumishi wa umma wawili wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

Akizungumzia ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Juma Makanya amesema magari hayo yamegongana leo eneo la Izazi wilayani Iringa ambapo gari aina ya Toyota Hilux mali ya TARURA yenye namba STL 3807 iliyokuwa ikiendeshwa na Lodrick Richard(35) ikitokea Iringa kuelekea Dodoma imegongana na gari aina ya Mistubishi Fuso namba T 146 BAZ mali ya Wilson Msenga .

Amesema gari hiyo ilikuwa inaendeshwa na Jumadin Mikata(32) mkazi wa Mbozi na kwamba katika ajali hiyo waliopoteza maisha ni dereva wa TARURA Lodrick Ricardh pamoja na Joyce Mlay (45) wakati waliojeruhiwa ni Ernest Mgeni, Gervas Myovela na  Jumadin Mikata.

"Miili ya marehemu imekadhiwa kwa Meneja wa TARURA katika Manispaa ya Iringa na  kuelekea Dodoma tayari kwa utaratibu  wa mazishi,"amesema.

Kuhusu chanzo cha ajali hiyo amesema ni uzembe wa dereva wa Fuso kushindwa kulimudu gari lake na kusababisha kuhama upande mmoja na kugongana uso kwa uso ambaye amekimbia baada ya ajali hiyo na sasa anatafutwa.

Ametoa  mwito kwa madereva kwa kuwa makini wanapokuwa barabarani na wasijione wako peke Yao bali waheshimu na watumiaji wengine wa barabara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...