Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
BENKI ya KCB Tanzania imezindua awamu ya pili ya programu ya 2jiajiri katika kuonesha dhamira ya dhati ya kumnyanyua mwanamke wa Kitanzania kujikwamua kiuchumi.

Warsha ya uzinduzi huo, iliyofanyika leo Juni 12, 2019 katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam imehudhuriwa na baadhi ya walengwa wa programu ya 2jiajiri, wafanyakazi wa Benki ya KCB, waandishi wa habari na wadau mbali mbali.

 Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Christine Manyenye amesema  benki hiyo inatarajia kutoa ruzuku ya jumla ya Sh. milioni 85 kwa jumla ya washiriki 17 watakaokuwa wamekamilisha na kufuzu awamu ya kwanza ya programu hiyo.

Amesema kuwa walengwa wanaotarajiwa kupata ruzuku hizo   watapitia mchujo ili kuhakikisha ustahili wa na matumizi sahihi ya ruzuku hiyo ili kukuza biashara zao na kuongeza ingawa ruzuku hiyo haina marejesho, benki ya KCB itaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya wapokeaji ili kuhakikisha wanawake hao wanafikia malengo yao ya kibiashara.

Aidha  Manyeye ameanisha vigezo ambavyo wapokeaji wanatakiwa kukidhi vikiwemo kujaza fomu inayopatikana katika tovuti ya Benki ya KCB na matawi yake nchi nzima.Pia  mpokeaji lazima awe amekamilisha mafunzo ya kinadharia na vitendo katika awamu ya kwanza na vie vile awe anaakaunti ya 2jiajiri iliyo hai na awe mwenye cheti na leseni halali ya usajili wa biashara. 

"Tangu kuzinduliwa kwa programu  hii mwaka 2016, benki imewawezesha wanawake 256 wa Tanzania katika sekta ya biashara na  kuwapa mafunzo mbali mbali na kuwapanulia wigo wa masoko ili kukuza mitaji na uwezo wa kibiashara ambapo kayi yao ni wanawake 115 ndio walipitia mafunzo kwa vitendo katika nyanja mbali mbali. 

Kwa upande wake, mnufaika wa programu hiyo,  Bhoke Mhini, Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Sekondari ya East Coast iliyoko Kibaha ambaye pia ni mmoja wa walengwa wa programu ya 2jiajiri amesema hajawahi kuona dhamira ya dhati katika kumuwezesha mwanawake wa Kitanzania. 

 Amesema kwamba  Benki ya KCB na 2jiajiri ni mfano wa kuigwa na taasisi nyingine kwani umenyanyua ufito wa uwekezaji kwa jamii. 
Mkuu Wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya  KCB, Christine Manyenye akizungumza na waaandishi wa habari wakati uzinduzi wa programu ya 2jiajiri ambapo jumla ya sh.milioni 85 zinatarajiwa kutolewa kwa wanawake 17 ili kukuza biashara zao, aliyekaa kushoto kwake ni Bhoke Mhini, mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya East Coast ya Kibaha, kulia kwake ni Rojas Mdoe, Mkuu wa kitengo cha uendeshaji na technology na mwishoni mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...