Na.Khadija seif,Globu ya jamii

*Hakuna ushindi wa janja janja
*Rashida wanjara kuwafunza warembo konki


KATIKA kurudisha fadhila kwenye sekta ya mitindo,Chuchu Hansy amejipanga kuratibu mashindano ya miss Tanga mwaka huu.

Akizungumza na Glovu ya Jamii msanii wa bongomovie ambae pia alikua miss Tanga mwaka 2005,Chuchu Hans amesema tayari amepewa vibali vyote vyakuendesha shindano hilo kuanzia kwa mratibu wa shindano la miss Tanzania Basilla Mwanukuzi pamoja na kibali kutoka baraza la sanaa (BASATA).

"Hii mi fursa ya kipekee kwa warembo kutoka mkoa wa Tanga kushiriki katika shindano hilo hivyo wachukue fomu mapema, na ni bure"

Hata hivyo chuchu ameeleza kuwa juni 6 mwaka huu fomu zitaanza kutolewa rasmi na mchakato wa mazoezi kwa watakaofanikiwa kuingia kambini yataanza 15julai ,na watahakikisha taji la miss Tanzania litakua zao la miss Tanga.

"Kwa sasa ni mapema mno kutaja zawadi kwa washindi ila washindi wategeme kitu cha tofauti na mashindano yaliyopita ,"

Aidha ametoa vigezo kwa washiriki kuwa awe mrembo anaejitambua ,yangi yake ya asili,mwenye akili timamu ambae ataweza kutuwakilisha vizuri ,hakuna ngono wakati kupendelewa atachaguliwa mrembo kutokana na kukidhi kwake vigezo.

Pia amesema warembo wataweza kujitolea kwenye jamii kuanzia kutangaza vivutio vya utalii vya mkoa wa Tanga.Kwa upande wake mkufunzi wa mashindano hayo Rashida wanjara amewasihi warembo kutoka mkoa wa Tanga kujitokeza kuchukua fomu.

"Nategemea kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa warembo watakaofanikiwa kupita katika mchujo wa kwanza ambao wataenda kambini rasmi kwa ajili ya kujipanga na kugombania ushindi huo mnono",

Wanjara amewatoa hofu washiriki kuwa ana uzoefu na tasnia ya urembo kwa miaka mingi kwani hata yeye alishawahi kuwa miss Tanzania mnamo mwaka 2000.
"Kupitia tasnia ya urembo nimeshawafundisha wengi akiwemo jokate,irene uwoya ,hamisa mobetto na wengine hivyo na uzoefu na kazi yangu ,"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...