Na EmanuelMadafa, MBEYA

JESHI la Polisi mkoani Mbeya, linamshikilia Daktari feki ajulikanaye kwa jina la Abdallah Bushiri (42) mkazi wa Igodima jijini Mbeya kwa tuhuma za kufanya kazi ya utabibu kwa kutibu magonjwa ya wanawake bila kuwa na taaluma ya udaktari.

Akizungumza na wandishi wa Habari jijini Mbeya , Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ulrich Matei amesema  mtuhumiwa alikamatwa Juni 24 mwaka huu nyumbani kwake.

Amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa kufuatia baadhi ya wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi hilo kuhusu shughuli anazofanya daktari huyo na akawekewa mtego uliowezesha kukamatwa na kupekuliwa nyumbani kwake.

Kamanda Matei amebainisha kuwa baada ya kupekuliwa nyumbani kwake, Daktari huyo feki alikutwa na vifaa tiba pamoja na dawa mbalimbali ambazo zinamilikiwa na Serikali zikiwa na nembo ya Bohari ya Dawa (MSD) pamoja a nembo inayoonyesha kuwa ni mali ya Serikali.

"Baada ya kumhoji tulibaini kuwa hana taaluma yoyote ya udaktari, lakini pia yuko na baadhi ya vifaa na dawa ambazo baadhi ni za Serikali, zina nembo ya MSD na GOT, lakini pia baadhi ya wananchi walikuja kulalamika kuwa mtu huyo alishachukua fedha zao zaidi ya 2,000,000," alisema Kamanda Matei.

Amesema  baadhi ya vitu alivyokutwa navyo mtuhumiwa huyo kuwa ni pamoja daftari 119 zenye taarifa za wagonjwa aliowahi kuwatibu, vipimo vya kupimia mkojo 15, dawa za kusafishia vidonda  kipimo cha Malaria ambacho kinapatikana MSD pamoja na vifaa vingine.

 Matei amesema kuwa baada ya taratibu kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria huku akiwataka wananchi wa Mkoa wa Mbeya kuendelea kutoa taarifa za uharifu na waharifu.

Mganga Mkuu wa Jiji la Mbeya, Dk. Jonas Lulandala aliwataka wananchi kuacha kwenda kutibiwa kwa watu ambao hawana taaluma ya udaktari kwa madai kuwa hali hiyo inaweza kuhatarisha maisha yao.

Aidha ametoa wito kwa  wananchi kutoa taarifa za watu wote wanaojifanya madaktari na kutoa huduma huku wakiwa hawana taaluma ya utabibu kama alivyofanya daktari feki aliyenaswa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...