SERIKALI Kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa la maendeleo la Japan (JICA) kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, imefanya mapitio ya mwongozo yakinifu wa Umwagiliaji unaolenga kufanya mabadiliko na maboresho katika kilimo cha Umwagiliaji nchini. 

Bw. Anthon Nyarubamba ni Meneja Msaidizi wa Mradi wa kujenga uwezo (TANCAID) kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji amesema hayo leo Mjini Morogoro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa kikosi kazi wa kupitia mwongozo huo. 

Bw. Nyarubamba alisema kuwa, mwongozo huo ambao ulikuweo tangu mwaka 2010 ambao ulikuwa katika mfumo wa kitabu kikubwa utaboreshwa na kuwekwa katika lugha rahisi na rafiki kwa watumiaji ambao ni wataalam, wakulima na wadau wote katika sekta hiyo, ambao utarahisisha na kuonyesha matumizi sahihi ya maji katika skimu za kilimo cha umwagiliaji. 

“Kabla ya kuwepo kwa Mwongozo huu wakulima wengi walikuwa wanadhani kuwa kilimo cha umwagialiaji ni kilimo chenye kutumia maji mengi lakini Mwongozo sasa utaonyesha matumizi sahihi ya maji sambamba na kujenga uwezo kwa wataalam na wakulima nchini.” Alisema Nyarubamba. 

Aidha Bwana Nyarumbana aliendelea kusema kuwa, mtu yeyote atakayeshughulika na kilimo cha umwagiliaji nchini atatakiwa kuufuata mwongozo huo ambao pia utachangia skimu za kilimo cha umwagiliaji nchini kujengwa katika ubora. 

Awali, Akiongea na waandishi wa Habari baada ya sehemu ya kwanza ya mapitio ya mwongozo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Ronald Komaga amesema tangu kuwepo kwa mwongozo huo mwaka 2010 kumejitokeza changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na kitabu cha mwongozo huo kuwa kikubwa na siyo rafiki kwa watumiaji, mwongozo kutoeleweka kwa wadau wengi na baadhi ya vipengele kutotekelezeka jambo ambalo limepelekea kuwa na awamu hii ya pili ya mapitio na maboresho ya mwongozo huo. 

Pamoja na changamoto hizo Bw. Komanga amesema kuwa Mwongozo wa awali pia ulitumika katika skimu nyingi za kilimo cha umwagiliaji zilizopo katika mradi na kuongeza uzalishaji hasa wa zao la mpunga. 

Kikosi kazi hicho chenye kufanya mapitio na maboresho ya mwongozo huo wa kilimo cha umwagiliaji umehusisha washiriki kutoka Serikali za Mitaa, Ofisi za kanda za Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, na wawakilishi kutoka JICA. 
Bw. Ronald Komanga Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, akiongelea mafanikio ya Maboresho ya Mwongozo yakinifu wa Kilimo cha umwagiliaji.
Katika Picha Bwana Anthon Nyarubamba ni Meneja Msaidizi wa Mradi wa kujenga uwezo (TANCAID) kutoka Tume a Taifa ya Umwagiliaji akiongea na waandishi wa Habari kuhusu mwongozo wa Umwagiliaji. (Habari na Picha Kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Morogoro) 

Sehemu ya washiriki (kikosi kazi) katika mkutano wa mapitio ya mwongozo yanikifu wa kilimo cha umwagiliaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...