Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

MFANYABIASHARA Andres Uribe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka moja la  kusafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine Hydrochloride.

Uribe amefikishwa mahakamani hapo leo Juni 17, 2019 ambapo amesomewa shtaka lake mbele ya Hakimu Mkazi, Augustine Mmbando.

 Wakili wa Serikali, Gloria Mwenda amedai kuwa Agosti 11, 2014 katika Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere (JNIA), mshtakiww alisafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine Hydrochloride zenye uzito wa gramu 904.7 ambayo yana thamani ya Sh milioni 63.3.

Hata hivyo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya.
Kwa mijibu wa upande wa mashitaka,  upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na  kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai Mosi, mwaka huu kwa kutajwa na mshitakiwa amerudishwa rumande.
 MFANYABIASHARA Andres Uribe alipofikishwa  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo  akikabiliwa na shtaka moja la  kusafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine Hydrochloride.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...