Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo ameelekeza Wataalam wa Sekta ya Maji mkoani Njombe kuanza kutumia pampu za kusukuma maji zilizobuniwa na Mzee John Fute zenye uwezo wa kusukuma maji kwa umbali wa zaidi ya mita 200 kulingana na mahitaji ya mteja bila kutumia umeme.
Mhandisi Kalobelo ametoa maelekezo hayo kwa wataalam hao akiwa mkoani Njombe kwa kuwataka wafanye uchunguzi wa kupata vyanzo vya maji vinavyoweza kutumia pampu za aina hiyo ndani ya wiki moja kuanzia Juni 17, 2019 kwa lengo la kuachana na gharama kubwa za umeme zinazochangia miradi mingi ya maji vijijini kutofanya vizuri.
‘‘Pampu za aina hii zinahitajika sana kwenye Sekta ya Maji kwa sasa kwa kuwawezesha wananchi walio mbali na mifumo ya miradi mikubwa ya maji kufikiwa na huduma kwa gharama nafuu kuanzia Shilingi 300,000 kulingana na mahitaji ya mteja. Tutashirikiana na COSTECH tufanye utaratibu wa kuziboresha tuanze kuzitumia mara moja.
Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Kalobelo ameambatana na timu ya wataalam wa Sekta za Maji, Nishati na Elimu kwa dhumuni la kutoa ushauri na kuona namna bora ya kuongeza tija kwa wabunifu wa umeme John Fute na Lainery Ngailo   kulingana na maelekezo ya Mhe. Rais, Dkt. John Magufuli aliyoyatoa Julai 13, 2019 kwa taasisi husika za Serikali mara baada ya kukutana na wabunifu hao Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Wabunifu hao wa kuzalisha umeme kutoka mkoani Njombe wamejikita katika kazi ya uzalishaji umeme kwa kutumia nguvu za maji na teknolojia ya uundaji wa pampu za maji.

 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo akizungumza na John Fute (kulia) mtaalam wa uzalishaji umeme kwa kutumia nguvu za maji na teknolojia ya uundaji wa pampu za maji, mkoani Njombe.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo akiwa na timu wa wataalamu wa Sekta ya Maji, Nishati na Elimu kwenye eneo la kazi la wabunifu John Fute na Lainery Ngairo, mkoani Njombe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...