NA TIGANYA VINCENT
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inaendelea na zoezi la kuhakiki  kwa viongozi wote wa Umma wanaojaza fomu  za tamko la rasilimali na madeni  ili kuepusha mgongano  wa maslahi miongoni mwao.
Kauli hiyo imetolewa leo na  Kamishna wa  Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma  Jaji Mstaafu Harold Nsekela wakati wa Mafunzo na maelekezo ya maadili ya siku moja kwa Viongozi wa Umma wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora na Manispaa ya Tabora.
Aidha Mh Nsekela amewata Viongozi hao kufanya kazi kwa Uadilifu kwa kufuata Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 ambayo inawataka Viongozi wa Umma kutekeleza Majukumu yao kwa Maslahi ya Taifa.
Alisema lengo ni kutaka viongozi wa umma wafanye kazi kwa kuzingatia maadili na kuweka maslahi ya Taifa mbele badala ya maslahi binafsi.
Mh Jaji Nsekela katika hotuba yake aliongeza kuwa mgongano wa maslahi kwa baadhi ya viongozi wa umma unaweza kulisababisha Taifa hasara ya kuwa na miradi inayotekelezwa chini ya viwango.
Katika hatua nyingine Kamishna huyo wa  Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma aliwataka viongozi wote wanaohusika katika ujazaji wa fomu  za tamko la rasilimali na madeni  kutenga muda wa kutosha kujaza fomu zao kwa ufasaha.
Alisema mara nyingi Viongozi wanaojaza fomu  za tamko la rasilimali na madeni wamekuwa wakisubiri siku za mwisho ndio wanaanza kujaza , jambo ambalo linaweza kusababisha kuachwa baadhi ya mali bila kuorodheshwa katika fomu hiyo ya Tamko.
Aliongeza kwamba Kiongozi wa Umma kujaza fomu za Tamko la Raslimali na Madeni ni takwa la Kisheria na ni lazima wala sio ombi. Na kwamba Kiongozi asipojaza fomu hizo na kuzirejesha kwa Kamishna wa Maadili kwa wakati ni kosa la kimaadili kisheria.
Alifafanua kwamba Kiongozi wa Umma anatakiwa kutoa Tamko lake la Raslimali na Madeni yake kila mwaka ifikapo mwishoni mwa Mwaka yaani tarehe 31 Desemba ya kila mwaka.
Mafunzo haya ya Maadili yamehudhuriwa na  Viongozi wa Umma wa Manispaa  zaidi ya Tabora  zaidi ya 200 wakiwemo Wakurugenzi, Makamanda wa polisi na jeshi la wananchi, wakuu wa wilaya, Madiwani, wakuu wa Idara na Vitengo
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua leo Mafunzo na maelekezo ya maadili ya siku moja kwa Viongozi wa Umma wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora na Manispaa ya Tabora.
 Kamishna wa  Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma  Jaji Mstaafu Harold Nsekela akitoa elimu  leo wakati wa mafunzo na maelekezo ya maadili ya siku moja kwa Viongozi wa Umma wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora na Manispaa ya Tabora.

Kamishna wa  Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma  Jaji Mstaafu Harold Nsekela akitoa elimu  leo wakati wa mafunzo na maelekezo ya maadili ya siku moja kwa Viongozi wa Umma wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora na Manispaa ya Tabora.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo na maelekezo ya maadili ya siku moja kwa Viongozi wa Umma wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora na Manispaa ya Tabora.  

Picha na Tiganya Vincent


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...