Serikali ya Tanzania imehimizwa kuridhia mkataba wa shirika la kazi duniani (ILO) namba 189 uliosainiwa Juni 16, 2011 kwa lengo la kuhimiza maslahi na kazi zenye staha kwa wafanyakazi wa nyumbani duniani.

Kwa mantiki hiyo, nchi zilizoridhia mkataba huo zinaingia kwenye utekelezaji wa maadhimisho ya Siku ya Mfanyakazi wa Nyumbani duniani na hivyo kutoa fursa ya kuihamasisha jamii kulinda na kuheshimu nafasi ya mfanyakazi huyo muhimu katika jamii.

Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, shirika la kutetea haki za wafanyakazi wa nyumbani (WoteSawa) lenye makazi yake jijini Mwanza, limeadhimisha maadhimisho ya Siku ya Mfanyakazi wa Nyumbani yaliyofanyika katika viunga vya Kishimba jumapili Juni 16, 2019.

Akizungumzia maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa shirika hilo, Angel Benedicto alisema ni wakati mwafaka sasa Serikali ya Tanzania kuridhia mkataba huo ili kuitambua rasmi Siku ya Mfanyakazi wa Nyumbani Duniani na kuiadhimisha ili kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kulinda maslahi ya kada hiyo tofauti na ilivyo kwa baadhi ya maeneo ambapo bado wafanyakazi wa nyumbani wanakumbana na changamoto kadhaa ikiwemo maslahi duni.Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Baadhi ya wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza wakiingia kwenye viunga vya Kishimba kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Mfanyakazi wa Nyumbani Duniani 2019.
Wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza wakionyesha jumbe mbalimbali kupitia mabango.
Wageni waalikwa meza kuu wakisoma jumbe mbalimbali kupitia mabango ya wafanyakazi wanyumbaji jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza walihimiza kulipwa ujira wao kwa wakati na kwa mujibu wa sheria ambapo kima cha chini ni shilingi elfu 40 kwa mwezi.
Baadhi ya wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Baadhi ya wafanyakazi wa nyumbani wakifuatilia maadhimisho hayo.
Jamii inahimizwa kutowaajiri watoto kufanya kazi za nyumbani na badala yake kuwapa fursa ya kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu.
Baadhi ya wazazi na walezi (waajiri) wa watoto wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza wakifuatilia maadhimisho hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kutetea haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani (WoteSawa), Angel Benedicto akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Mfanyakazi wa Nyumbani yaliyoandaliwa na shirika hilo jijini Mwanza.
Tazama Vidio hapa chini

Wafanyakazi wa Nyumbani Mwanza wasisitiza maslahi yao kuzingatiwa
Waajiri wajitokeza kuhimiza haki za wafanyakazi wa nyumbani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...