Na Ahmed Mahmoud, Arusha 

Taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru (TICD) imezindua bonanza la michezo kwa wanafunzi na watumishi wa taasisi hiyo yakiwa na lengo la kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli pamoja na kumpongeza kwa kazi nzuri anayofanya katika kuelekea uchumi wa viwanda. 

Akizungumza jana wakati wa kuzindua bonanza hilo lenye jina la TICD maendeleo bonanza 2019,Kaimu mkuu wa chuo hicho, Dokta Bakari George alisema kuwa, lengo la bonanza hilo lenye kauli mbiu ya “vijana nguvu kazi ya Taifa kufikia uchumi wa kati “ni kumuunga mkono na kumpongeza Rais Magufuli katika juhudi nzuri anazofanya katika kuelekea uchumi wa viwanda . 

Dokta Bakari alisema kuwa, wamekuwa wakihamasisha michezo chuoni hapo kila mwaka kwa lengo la kuunganisha mahusiano mazuri kati ya watumishi wa taasisi hiyo pamoja na wanafunzi sambamba na kuibua vipaji mbalimbali. 

Alisema kuwa, bonanza hilo limekuja muda muafaka ambao wanafunzi wanaelekea katika mitihani ambapo itawawezesha kuwandaa vyema katika kufanya vizuri ikiwa ni pamoja na maandalizi ya timu ya taasisi hiyo kujiandaa katika kushiriki mashindano ya michezo ya vyuo vikuu mwezi wa kumi yatakayofanyika jijini Mwanza. 

“bonanza hili litasaidia pia kuinua vipaji mbalimbali vya wanafunzi wetu katika kuipenda michezo wakiwa tangu wadogo ,kwani kuna wanafunzi wengi wana vipaji vizuri katika michezo mbalimbali hivyo wanahitaji kujengewa uwezo kama hivi ili waendelee kuipenda michezo hiyo. “alisema Dokta Bakari. 

Mhadhiri na Mratibu wa michezo hiyo katika taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru, Elifadhili Mpehongwa alisema kuwa, wamekuwa wakifanya Bonanza hilo kila mwaka ambapo huu ni mwaka wa tatu kufanya bonanza hilo ambapo limekuwa na manufaa makubwa hasa kujenga mahusiano mazuri kati ya watumishi na wanafunzi. 

Alisema kuwa, bonanza hilo limeshirikisha timu 6 ambapo timu 5 ni za wanafunzi huku timu moja ikiwa ya watumishi wa taasisi hiyo na imeshirikisha michezo ya mpira wa miguu, mpira wa Pete, mpira wa wavu, drafts na mpira wa pool table ambapo mwisho wa siku ni kuweza kupata wataalamu wazuri waliobobea katika michezo mbalimbali. 

Aliongeza kuwa, lengo la bonanza hilo pia ni kuweza kuufufua mchezo wa draft ambao umesahaulika Sana na una historia kubwa katika nchi yetu na unahitaji kuendelezwa kwa kasi kwani ni mchezo ambao hautumii nguvu na unachezwa na watu wa umri wowote. 

“katika bonanza hili mshindi wa kwanza atapatiwa mbuzi wawili, huku mshindi wa pili na wa tatu wakipatiwa mbuzi moja moja na tumefadhiliwa na kampuni ya bia ya Heineken kupitia kinywaji chake chake cha Aimstell ambao wameahidi kuendelea kutusaidia zaidi katika michezo mbalimbali. “alisema Mpehongwa. 

Mmoja wa wachezaji wa mpira wa miguu, Yohana Makala alisema kuwa, uwepo wa michezo hiyo kwenye vyuo inasaidia Sana kuweka mahusiano ya karibu kati ya watumishi na wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuwawesha wanafunzi kujiepusha na makundi mbalimbali yasiyofaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...