Namba ya Zabuni: KMA/2019/2010/UJ/01
Kwa ajili ya:-
Ujenzi wa majengo ya shule tarajali ya King Mansa Academy: Likokona-NANYUMBU, Mtwara.
- Taasisi ya King Mansa Academy inakaribisha maombi kutoka kwa mtu binafsi, makampuni, taasisi au vikundi mbalimbali ili kujenga majengo ya shule tarajali eneo lililoko Likokona- Nanyumbu.
- Unakaribishwa kununua nyaraka za zabuni na kupata maelezo kwa Katibu wa bodi ya zabuni ya King Mansa Academy ya Likokona- Nanyumbu. Ofisi ziko barabara ya kuelekea Chuo Kikuu cha Maji inaitwa KGSS stationery. Ofisi ziko wazi kuanzia saa saa2 asubuhi hadi saa11 jioni kila siku isipokuwa Jumapili na sikukuu.
- Ujenzi utakaofanyika utakuwa kama ifuatavyo:
LOT: 1- Ujenzi wa jengo la utawala.
LOT: 2- Vyumba 16 vya madarasa.
LOT: 3- Ukumbi wa matumizi mchanganyiko (Multipurpose Hall) na ujenzi wa jiko.
LOT: 4- Kuchimba kisima kirefu (drilling a borehole).
LOT: 5- Nyumba 5 za watumishi (two in one).
LOT: 6-Vyoo matundu 40.
Tender document iandikwe kwa lugha ya Kiingereza.
- Ada ya zabuni ni Tsh 100,000/= fedha ambayo haitarejeshwa. Malipo hayo yafanyike kwa akaunti ya NMB 60310009133 yenye jina Mansa Nyuchi. Utakatiwa risiti kuonyesha imepokelewa na bodi ya zabuni ili kupatiwa kitini ‘pamphlet’ ya zabuni unayoomba.
- Bahasha zenye zabuni, halisi moja na nakala moja, zifungwe kwa makini zikionyesha Jina la namba ya zabuni. Kisha zirudishwe kwa Katibu ofisi za KGSS stationary.
- Kwa maelezo wasiliana na:
Katibu wa Bodi ya Zabuni
King Mansa Academy
S.L.P 700- Dar es Salaam
Simu: 0767 044068, 0787 044068, 0717 632885
Mwombaji ataje kiasi cha fedha katika zabuni aliyoomba.
- Siku ya mwisho ni tarehe 28/6/2019 saa 4:00 asubuhi. Kabla ya ufunguzi utakaofanyika hadharani katika ukumbi wa Princess Hall ulioko Mapambano – Sinza, unaruhusiwa kuleta Mwakilishi.
- Zabuni zifuatazo hazitakubaliwa:
- Zabuni zilizochelewa,
- Zabuni za kielektoniki au
- Zabuni zisizofungwa.
.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...