Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa changamoto ya mawasiliano ni watumiaji wenyewe kwa kutojua namna ya kutumia mitandao.

Odiero aliyasema hayo jana wakati akifungua mkutano wa Kanda ya Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa mkutano wa wadau ni kutaka kupata ushauri na changamoto ya mawasiliano katika utoaji huduma unaofanywa na TCRA Kanda ya Mashariki.

Mhandisi Odiero amesema kuwa kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wadau ikiwa ni utoaji wa maoni pamoja na changamoto zinazowakabili ambazo baada ya mkutano huo zitashugulikiwa.  Aidha amesema kuwa mkutano huo ni pamoja na kujua mkataba wa TCRA katika utoaji huduma ikiwa na watoa huduma kutoa mkataba kwa wateja wao kwa bidhaa wanazozipata.

Odiero amesema kuwa malalamiko walioyapokea ni 57 ambapo wanashughulikia  yanayohusiana na matumizi ya simu. Mmoja wa wadau meneja wa Abood Media Abeid Dogori amesema  kuwa mkutano wadau ni mhimu kwani unatatua changamoto kwao kwa kutoa yaliyomoyoni na kuwa tofauti na kupeleka taarifa kwa maandishi.

Amesema kuwa TCRA imejapambanua katika utoaji huduma kwa wateja wao ikiwa ni kutatua changamoto kutokana na kushirikisha baadhi vyombo vingine vya serikali ikiwemo Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Jeshi la Polisi.

Meneja wa Radio Okoa FM ya mkoani Morogoro Gelard Nyabinyili amesema kuwa TCRA iendelee kuwa karibu ili changamoto zinazowakabili kama watoa huduma kuweza kutatuliwa kwa wakati.

Amesema jambo la kuleta mkataba kwa  mteja wa TCRA ni muhimu kwani wangeweza kukaa nao lakini wameona ushirikishaji ni bora kwa wateja kuelewa katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza katika kukaa cha wadau wa sekta ya mawasiliano Kanda hiyo kujadili changamoto za Kihuduma na kiudhibiti kwa lengo la kuboresha sekta kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Radio ya Okoa FM ya mkoani Morogoro Gelard Nyabinyili akitoa maelezo mara baada ya kupata leseni katika kikao cha wadau wa mawasiliano kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero (katikati) akiwa na watendaji wa TCRA wakisiliza ushauri unaotolewa na wadau wa mawasiliano katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi  Lawi Odiero akimkabidhi Leseni Meneja wa Radio ya Okoa FM Gelard Nyabinyili  katika kikao cha wadau kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi wadau wa mawasiliano wakiwa katika kikao kilichoratibiwa na Kanda ya Mashariki ya TCRA na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...