Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kyerwa umefikia aslimia 85 kukamilika, hii ni kutokana na muda uliopangwa kukamilika kwa Hospitali zote zinazojengwa Wilayani kukamilika ifikapo Juni 30.

Akisoma taarifa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, ambaye amefika hospitalini hapo kujionea hatua ya ujenzi huo, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Dkt. Diocles Ngaiza amesema licha ya Ujenzi wa hospitali hiyo kuendelea vizuri kwa baadhi ya majengo kufikia hatua za mwisho kabisa, ametaja changamoto kubwa kuwa ni ongezeko la vifaa vya ujenzi tofauti na (BOQ) lakini pia jengo moja ambalo hapo awali TAMISEMI walikosea mchoro wake, na sasa jengo hilo linaendelea kwa kasi baada ya kurekebishwa mchoro huo.

Aidha Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti ameridhishwa na kazi nzuri inayoendelea, kwa usimamizi mzuri chini ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Kamati zake, huku akiongeza kuwa kazi inayoonekana ni sawa na thamani ya kiasi cha pesa ambacho tayari kimekwishatumika.

Katika kuhakikisha shughuli ya ujenzi wa hospitali hiyo unakamilika haraka na kwa muda. Mhe. Gaguti ametoa muda wa siku kumi awe amekabidhiwa majengo yote ya hospitali hiyo yakiwa yamekamilika kwa asilimia mia moja.

Akitoa shukrani zake kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Jinsi ambavyo ameupendelea Mkoa wa Kagera kwa kuuzawadia Hospitali tatu za Wilaya, zikiwemo zile zinazojengwa katika Wilaya za Karagwe na Bukoba. 
 Pichani ni baadhi ya majengo kati  ya majengo saba ya  hospitali ya Wilaya ya Kyerwa yakiwa yamefikia hatua za mwisho za ujenzi.
 Pichani ni baadhi ya majengo kati  ya majengo saba ya  hospitali ya Wilaya ya Kyerwa yakiwa yamefikia hatua za mwisho za ujenzi.


 Pichani ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Diocles Ngaiza akisoma taarifa ya Ujenzi wa Hospitali ulipofikia wakati Mkuu wa Mkoa Kagera alipofanya ziara ya kukagua Ujenzi huo.

 Pichani ni msafara wa Rc Gaguti pamoja na Uongozi wa Wilaya ya Kyerwa wakiendelea na ukaguzi wa majengo ya Hospitali mpya ya Wilaya ya Kyerwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...