Na.Vero Ignatus,Arumeru

Vijana wametakiwa kuhakikisha wanarudisha mikopo yote waliyokopeshwa kwenye vikundi vyao ili kusaidia kukuza mfuko wa Wazira na kutoa fursa ya vikundi vingine kukopeshwa.

James Kajugus ni Mkurugenzi wa idara ya vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,ajira,vijana na watu wenye ulemavu, ametoa maelekezo hayo alipokuwa akitembelea vikundi mbalimbali vya vijana katika 
halmashauri ya Meru.

Amesema Wizara kupitia mfuko wake wa maendeleo ya vijana ulitoa kiasi cha fedha Milioni 103 kwa halmashauri ya Meru kwa lengo la kukopesha vikundi mbalimbali vya vijana vinavyofanya shughuli za maendeleo na ukuzaji wa uchumi.

“Nashangwazwa sana na taarifa hii ya vikundi vingi vya vijana kupata 
fedha za serikali lakini wameshindwa kurejesha na hata Saccoss ya vijana 
Meru ambayo ndio inasimamia fedha hizo imeshindwa kuvifuatilia vikundi 
hivi ili virejeshe mikopo hii”.

Amesisitiza zaidi juu ya fursa mbalimbali zinazotolewa na Wizara kupitia 
idara ya vijana mbali na mikopo kuwa ni fursa za kuongeza ujuzi kwa 
vijana wabunifu ambao hawajasomea na fursa za mafunzo mbalimbli kwa 
vijana.

Akielezea changamoto zinazosababisha vikundi vya vijana kushindwa 
kurejesha mikopo Mkurugenzu Mtendaji wa Halmashauri ya Meru bwana 
Emmanuel Mkongo, amesema vijana wengi hawaaminiani kwenye vikundi 
vyao na hiyo kupelekea vingi kuvunjika au wanavikundi kukimbia na 
mikopo hiyo

Pia, amesema kuna hali ya siasa kuingilia ufuatiliaji wa fedha hizi za 
mikopo na hivyo kufanya mazingira ya urejeshaji kuwa magumu zaidi na 
baadhi ya vikundi vya vijana kuingia kwenye siasa hizo.Aidha, amesema mbali na changamoto hizo bado halmashauri yake kushirikiana na maafisa husika wanaendelea kuhakikisha fedha zotezilitolewa na Wizara na halmashauri zinarejeshwa ili kutoa nafasi ya vikundi vingine kunufaika pia.

Nae mwenyekiti wa kikundi cha Old is Gold Arts group bwana Samola Mloe, 
amesema mikopo ya vijana inayotolewa na Wizara imesaidia sana kikundi 
chao kukua na mafunzo waliyopewa na halmashauri yamewasaidia pia 
kupata masoko kupitia mitandao ya kijamii nje ya nchi.

Bwana Kajugusi yupo katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Arusha kwa 
lengo la kutembelea vikundi mbalimbali vya vijana na kukagua miradi ya 
maendeleo inayofanywa na vikundi hivyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana bwana James Kajukusi(mwenye suti nyeusi)akisisitiza jambo kama anavyoonekana katika picha.

Mkurugenzi wa Idara ya Vijana bwana James Kajukusi(mwenye suti nyeusi) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Emmanuel Mkongo katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...