Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WIZARA ya Fedha na Mipango imewataka wadaiwa sugu wa madeni ya Commodity Import Suport (CIS) na Na Food Aid Counterpart Fund (FAFC) wakiwemo wafanyabishara maarufu nchini Yusuph Manji na Mohamed Dewji 'MO' kuhakikisha wanalipa madeni hayo mara moja.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James katika tangazo la wadaiwa hao iliyotolewa leo Juni 19, 2019 kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Wizara ya Fedha na Mipango inawataka wadaiwa sugu wa madeni hayo kuhakikisha wanalipa mara moja na kwamba licha ya kutolewa tangazo la awali bado wameshindwa kuitikia mwito.

"Madeni haya ni mkopo wenye masharti nafuu yaliyotolewa kwa Taasisi, Kampuni, Viwanda na Wafanyabiashara,  ambapo wakopaji walitakiwa kulipa deni bila kutozwa riba katika kipindi cha Miezi 18 tangu walipopewa mikopo hiyo.

"Kwa mujibu wa sheria ya CIS (The Commodity Import Support Regulation Act, CAP 261 R. E. 2002 (s.8 (1)(b), Mkopaji akichelewa kulipa katika kipindi cha miezi 18 tangu kupatiwa mkopo, atapaswa kulipa riba ya asimilia sawa na kiwango kinachotozwa na Benki Kuu ya Tanzania inapoikopesha Serikali katika kipindi husika. Zaidi ya makampuni 980 yalikopeshwa chini ya utaratibu huu,"amesema James kwenye  taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa  Wizara hiyo, Wizara hiyo imesema kuwa Serikali inatangaza kwa mara ya mwisho kutokana na baadhi ya wadaiwa ambao wameshindwa kuitikia mwito wa matangazo ya awali ya Desemba 30 mwaka 2015 na Aprili 5 mwaka 2018. 

 "Hatua za kisheria zitachukuliwa mara baada ya kutoka kwa tangazo hili,"amesema.

Katika orodha ya kwanza ya wadaiwa sugu wa madeni yatokanayo na mkopo huo ni Yusuph Manji aliyekopa kupitia kampuni zake za  Farm Equipment Tanzania Ltd,   Quality Group Ltd,  Dunhill Motors Ltd, Quality Seed Ltd na Quality Garage Ltd  na Mohamed Dewji kupitia   21st Century Textiles Ltd na Afritex Ltd

Mdaiwa mwingine ni  S. S Rashid kupitia   Pwani Tours and Safari Ltd na Pwani Investment Ltd. Pia Issack Bugali kupitia Dar es Salaam International School Trust Fund na  Upoloto Farm  Ltd.Pia yumo K.B Medicare Ltd (Prof. Bernard Kirei), Siza Cold Storage Co.Ltd (Stephen Wasira)

8. Sorority Co. Ltd (Martha Lyimo)  21st Century, Afritex Ltd,na  Kichonge Miller (Bokeye Kangoye)

Wadaiwa sugu wengine ni Rela Investment Company Ltd (Ahiya E. Lukumayi), Bahari Motor Co Ltd (Hashim Rungwe), Andrew Traders Co Ltd (Andrew Richard Kisenge), Oth Investment Co Ltd (Boniventure Boniventure)
na Kiomboi Kisiriri Pharmacy Ltd (Dkt Kingu) 

Wizara hiyo imesema kwa maelezo zaidi imewataka wadaiwa hao kuwasiliana na Kikosi Kazi, Wizara ya Fedha na Mipango, Dar es Salaam, chumba Na. 352, Simu Na. +255 739403025/ 2122282285

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...