Na Said Mwishehe,Michuzi TV

KIWANDA cha A to Z cha mkoani Arusha kimewashauri Watanzania kununua bidhaa zinazolishwa na viwanda vya ndani ili kuijenga Tanzania pamoja hasa kwa kuzingatia viwanda vya ndani vinatengeneza bidhaa bora kuliko zinatoka nje.

Kiwanda hicho ambacho kimeshika nafasi ya kwanza kwa kuzalisha bidhaa bora katika Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa kwa mwaka 2019.

Akizungumza wakati anazungumza na Michuzi TV na Michuzi Blog katika maonesho hayo yanayoelekea kumalizika Shom Darlami kutoka A to Z amesema wanajivua bidhaa bora ambazo zinatengenezwa na Watanzania zaidi ya 8000 waliopo kiwandani hapo.

Hata hivyo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa A to Z inatamani na kuona bidhaa za Tanzania zikipewa kipaumbele kwa kununuliwa na Watanzania wenyewe na kwa kufanya hivyo usaidia kwanza kutafanya wenye viwanda kuendelea na uzalishaji lakini pili itakuwa fursa ya kuijenga Tanzania ya viwanda kwa pamoja.

"Kwanza tueleze A to Z tunazalisha bidhaa bora kwa gharama nafuu.Hata hivyo tunashauri wananchi wote wawe na utamaduni wa kupenda kununua bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vya Tanzania.

"Viwanda vya Tanzania kikiwemo A to Z  tunazalisha bidhaa bora sana kuliko hata hizo bidhaa zinazotoka katika nchi nyingine na kuingizwa nchini.Watanzania tupende vya kwetu ili kuijenga nchi yetu kwa pamoja na hatimaye kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya tano katika kuelekea uchumi wa kati utokanao na viwanda,"amesema Darlami.

Kuhusu kiwanda chao amesema katika maonesho ya biashara ya 43 kimeshika nafasi ya kwanza katika utengenezaji wa bidhaa bora huku akieleza kufurahishwa na idadi kubwa ya wananchi ambao wamekuwa wakifika kwenye banda la A to Z kununua bidhaa za nguo.

"Ahadi yetu ni kuendelea kuzalisha bidhaa bora kama kawaida yetu na kwa gharama nafuu.Ubora wa bidhaa zetu umetufanya tusiwe tunatangaza sana katika vyombo vya habari kwani akija mtu akanunua bidhaa yetu basi huyo atakwenda kuwaambia na wengine tena mdomo kwa mdomo na matokeo yake bidhaa zetu zinapendwa na tunapata wateja wengi sana,"amesema.

Amesisitiza kuwa ubora wa bidhaa zao unatokana na ari ya kazi kutoka kwa wafanyakazi wazawa 8000 ambao wameajiriwa kiwandani hicho kuhakikisha uzalishaji bidhaa unafanyika na tena kwa kiwango chenye ubora wa hali ya juu.

"Kila mwaka tunaona watu wanavyoongezeka katika kununua bidhaa zetu,"amesema Darlami na kuongeza wamekuwa na utaratibu wa kutangaza bidhaa zao mara moja tu kwa kila mwaka kupitia maonesho hayo na baada ya hapo huduma zao zinapatikana moja kwa moja kutoka kiwandani kwao.

"Baada ya maonesho haya tunarudi kiwandani, hivyo wanaohitaji bidhaa zetu tunawahudumia kutoka kiwandani.Kutokana 3na ubora wa bidhaa zetu tumekuwa tukifuatwa kokote tulipo na hasa kiwandani,"amesema.

Alipoulizwa ni aina gani ya bidhaa ambazo zimenunuliwa sana katika maonesho hayo ya biashara, amejibu nguo za watoto zimenunuliwa sana pamoja na nguo za wanawake.
 Baadhi ya bidhaa za nguo zinazozalishwa na viwanda cha A to Z mkoani Arusha zikiwa zimepangwa kwenye maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wananchi wakiendelea kuchagua nguo katia banda la A to Z katika maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Shoma Darlami akiwa ameshika  fulana ambayo imenunuliwa na moja ya wateja waliofika katika banda la A to Z katika maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Shom Darlami akionesha moja  fulana ambayo inatengenezwa na kimwanga cha A to A cha mkoani Arusha katika maonesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam
Muonekano wa banda la A to Z Katika maonesho ya biashara ya 43 ya Kimataifa jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...