Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Siku moja baada ya Rais John Pombe Magufuli kuagiza kushugulikiwa kero ya Maji kwa wakazi wa Kyaka, Kata Burifani, na Kata jirani, katika Wilaya ya Missenyi, Waziri wa Maji Professa Makame Mbarawa amefika Wilayani humo ili kuanza utekelezaji wa agizo hilo.

Akiambatana na Safu ya wataalam mbalimbali wa Maji kutoka BUWASA na wengine kutoka Mwanza pamoja na Wizarani, amefika eneo la Kyaka na kufanya Mkutano wa hadhara ambapo katika mkutano huo ameahidi kuanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais kwa haraka ili kutatua kero hiyo ndani ya miezi mitano.

Aidha Professa Mbarawa amesema kuwa kwa sasa Wizara ya Maji imejipanga vyema kuhakikisha miradi ya Maji inatekelezwa na Wakandarasi wenye sifa na uwezo kwani kipindi cha nyuma miradi mingi ilikwama kutokana na Kandarasi wabovu, na kukiri kuwa uwepo wa ukiritimba na urasimu, ambapo watumishi wachache wasiokuwa waadilifu wamekuwa wakishirikana na wakandarasi wabovu kutekeleza miradi ya Maji isiyokuwa na Viwango, lakini sasa marekebisho makubwa yamefanywa na kuahidi usimamizi makini.

Itakumbukwa kuwa Mhe. Rais alitoa agizo la kumaliza kero ya maji eneo la Kyaka, wakati aliposimama eneo hilo kusalimia wananchi waliokuwa wakimsubiri barabarani, na baada ya kuelezwa kero hiyo alimpigia simu Waziri Mbarawa na kumtaka afike Mara moja kulishughulikia.
 Pichani Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na Wananchi wa Muleba na Tanzania wakati aliposimama Muleba Mjini, waliosimama ni Rc Gaguti, Dc Luyango, na Waziri Mbarawa
  Waziri Mbarawa akihutubia Wananchi na wakazi wa Kyaka alipowasili hapo tayari kuanza kutekeleza agizo la Rais juu ya utatuzi wa Kero ya Maji.
Pichani ni Timu ya wataalam, watumishi wakiongozwa na Waziri wa Maji Profesa Mbarawa wakiwa juu ya Kilima Rubale Kata Kyaka ambapo tanki kubwa la mradi wa Maji litajengwa hapo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...