Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akisalimiana na Meneja Mkuu wa Hoteli ya Kimataifa ya RIU Palace Zanzibar iliyopo Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja Bwana Luis Sanchez Sarda alipofika kukagua maendeleo ya ongezeko la ujenzi wa vumba vya kulala wageni.
Balozi Seif akiupongeza uongozi wa Hoteli ya RIU Palace Zanzibar kwa kujikita katika uwekezaji ndani ya Sekta ya Utalii na kuwatahadharisha kuepuka ujenzi wa majengo yao kutumia makuti. Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Mh. Vuai Mwinyi Mohamed na Meneja Mkuu wa Hoteli ya Kimataifa ya RIU Palace Zanzibar Bwana Luis Sanchez Sarda.
Muonekano wa haiba ya Baadhi ya Majengo mapya ya
vyumba vya kulala wageni ya Hoteli ya RIU Palace Zanzibar yaliyopo
Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewashauri
Wawekezaji wa Mahoteli katika Sekta ya Utalii Nchini kuzingatia
umuhimu wa kutoa fursa za ajira kwa Wazawa ili kudumisha mahusiano
mema katika uendelezaji wa Miradi yao.
Alisema hatua hiyo itakwenda sambamba na azma ya Serikali Kuu katika
kufungua Milango ya Uwekezaji itakayoshajiisha fursa zaidi za ajira
hasa kwa Vijana itakayosaidia kupunguza msongamano wa makundi yasiyo
na Kazi Mitaani.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa ushauri huo wakati wa ziara yake ya
kuangalia maendeleo ya ongezeko la Ujenzi wa vyumba vya kulala Wageni
katika Hoteli ya RIU Palace Zanzibar iliyopo Nungwi Mkoa wa Kaskazini
Unaguja.
Alisemaongezeko kubwa la Vijana wanaomaliza Masomo yao limekuwa kubwa
mno na kulazimika Serikali kubuni mbinu za kupambana na changamoto
hiyo iliyoenea hata katika Mataifa makubwa yaliyoendelea kiuchumi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameupongeza Uongozi mzima wa Hoteli
ya Kimataifa ya RIU Palace Zanzibar kwa uamuzi wake wa kutanua Mradi
wao jambo ambalo litaongeza mapato ya Taifa na kukuza fursa zaidi ya
Ajira.
Balozi Seif ameutaka Uongozi huo kuepuka uwezekaji wa makuti kwenye
majengo yao ili kujikinga na jaribio lolote linaloweza kusababishwa na
majanga ya moto hasa wakati wa kiangazi.
Alisema ipo miradi mingi ya Mahoteli iliyowahi kutumia mfumo huo wa
makuti kwa dhana ya kuridhisha Wateja wao lakini hatma yake imepunguza
uzalishaji na mengine kufungwa kabisa baada ya kupata majanga ya moto.
Mapema meneja Mkuu wa Hoteli ya Kimataifa ya RUI Palace Zanzibar Bw.
Luis Sanchez Sarda alisema Uongozi wa Hoteli hiyo umelazimika kuongeza
idadi ya vyumba vya kulala wageni ili kukidhi mahitaji ya Wateja wao
wanaoongezeka kila kukicha.
Alisema ongezeko la ujenzi huo utafikia vyumba 100 vya kulala wageni
vinavyojengwa katika mfumo wa vyumba 50 kwa kila awamu
vitakavyoiwezesha Hoteli hiyo kufikia idadi ya vyumba Mia 200.
Meneja Mkuu huyo wa RIU Palace Zanzibar alimuhakikishia Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar kwamba ujenzi wa vyumba hivyo uliofikia asilimia
85% sasa utakamilika rasmi ifikapo Mwezi Novemba Mwaka huu na kuongeza
idadi ya Wafanyakazi Wazawa 40.
Kwa upande wake Mkurugenzi Uwezeshaji na Miradi ya Uwekezaji kutoka
Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar {ZIPA} Shariff Ali
Shariff alisema mabadiliko ya Sheria ya Uwekezaji yaliyofanywa na
Serikali hivi karibuni inaelekeza Muwekezaji ye yote analazimika
kuwekeza Mradi wake Nchini usiopungua thamani ya Dola za Kimarekani
Milioni Mia Moja.
Shariff alisema uamuzi huo wa mabadiliko ya Sheria ya Uwekezaji
umezingatia umuhimu wa kuimarisha Miradi ya Kudumu ya Uwekezaji
itakayoendelea kutoa ajira kubwa, kuongeza mapato na kuimarisha Uchumi
wa Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...