NA Charles James, MICHUZI TV

MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia Nyamoga amesema kuna haja ya walimu wa timu za Taifa kuangalia vipaji ambavyo vinapatikana maeneo ya vijijini.

Hayo ameyatoa wakati akifunga mashindano ya Buchimwe Cup yaliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari Buigiri ambapo mchezo wa fainali ulizikutanisha timu za Buigiri Mission na Songambele.

Mkuu huyo wa Wilaya alisema vijijini kumekuwa na vipaji vya hali ya juu lakini anakosekana mtu wa kuwashika mkono hivyo akawaomba walimu wa timu za Taifa kuifika katika maeneo hayo.

“Waje na hapa kwetu Chamwino kuna vipaji vya hali ya juu naamini hata wale Algeria waliochukua AFCON kupitia vipaji hivi ninavyoviona hapa wasingeweza kutufunga,”amesema.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buigiri Mhe Kenneth Yindi ambaye ndie muandaaji wa mashindano hayo amesema ataendelea kuandaa mashindano mbalimbali ya Michezo wilayani humo ili kukuza vipaji vya vijana kwani Michezo imekua ni ajira kubwa iliyobadilisha maisha ya vijana wengi.

" Mhe DC tunakushukuru sana kwa kufika pamoja na kufanikisha mashindano haya bado tunakabiliwa haswa na uhaba wa viwanja pamoja na vifaa vya Michezo, tuwaombe Serikali kuwekeza Kwa nguvu pia huku vijijini ambapo tunaamini kuna vipaji vingi," amesema Mhe Yindi.

Katika fainali hiyo iliyohudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo la Chilonwa,Joel Mwaka (CCM),Buigiri Mission waliibuka na ushindi wa Penalti 3-1 dhidi ya Songambele mara baada ya dakika 90 timu hizo kutoka sare ya kutofungana.

Jina la mashindano hayo,Buchimwe ni muunganiko wa herufi za mwanzo za vijiji vitatu vilivyopo katika Kata ya Buigiri ambavyo ni Chinangali 11,Buigiri na Mwegamile.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe Vumilia Nyamoga akimkabidhi Kombe Nahodha wa Timu ta Buigiri Mission baada ya kutwaa taji la mashindano ya Buchimwe,

 Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe Vumilia Nyamoga akikagua kikosi cha Timu ya Songambele kwenye mchezo wa fainali wa mashindano ya Buchimwe Cup

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...