Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Mhandisi Atashasta Nditiye, amesema Ujenzi wa Jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) umekamilika, na Jengo linatarajiwa kuanza uendashaji mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.

Pia amesema amefurahishwa kwa kukamilika kwa jengo hilo ambapo ni la kisasa na huduma zake zake ni nzuri.

Akizungumza mara baada ya Ziara ya kukagua Jengo hilo , amesema katika idadi ya miruko ya ndege Barani Afrika JNIA inachukua nafasi ya tano na nafasi ya sita kwa idadi ya abiria.

‘’ Nimefurahishwa kwa kukamilika kwa Ujenzi wa jengo la tatu la abiria wa Kiwanja cha Ndege ambapo utakapoanza kuhudumia abiria natarajia tutachukua nafasi nzuri zaidi Barani Afrika kwani ni Jengo la kisasa na litatoa huduma nzuri,’’ alisema.

Nae Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere( JNIA), Paul Rwegasha akitoa ufafanuzi wa Kiwanja hicho, alisema mara baada ya kukamilika kwa jengo la tatu itakuwa jumla ya majengo matatu yanaweza kuhudumia abiria milioni nane kwa mwaka.

Rwegesha alisema ujenzi wa jengo la kwanza lina uwezo wa kuhudumia abiria 500,000 kwa mwaka na ujenzi wa jengo la pili abiria milioni 1.5

Alisema kukamilika kwa jengo hilo la tatu kutaongeza idadi ya Ndege, abiria pamoja na Watalii baada ya kuwa na Miundombinu bora na ya kisasa.

Vile vile alisema Ujenzi wa jengo la tatu ni kwa ajili ya abiria wa safari za Kimataifa ambapo kwa sasa yako mashirika 23 na jengo la pili kwa ajili ya abiria wa safari za ndani ya nchi huku jengo la kwanza safari za ndani pia. .

Alisema ujenzi wa jengo la tatu la abiria litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 2,800, kwa saa na maegesho ya magari mchanganyiko yasiopungua 2,075 kwa wakati mmoja.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama, alisema kwasasa kuna katika maandalizi ya Wakuu wa Nchi na Serikali watakaohudhuria mkutano wa 39 wa SADC ambapo maadalizi yameambatana na ukarabati wa maboresho ya miundombinu na samani.

Ndyamukama, alisema wageni hao wanatarajia kuingia hapa nchini Agosti mwaka huu ambapo watapata huduma bora zaidi na yenye uhakika.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa Viwanja vya Ndege Tanzania Mhandisi Julius Ndyamukama (mwenye koti jeusi)akisoma Taarifa ya Mradi wa Jengo la III la abiria kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye alipofanya ziara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye akihoji jambo katika Ukumbi wa Watu mashuhuri alipotembelea jengo la III la abiria.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Bw, Paul Rwegasha ( mwenye koti kijivu) Akitoa maelezo ya jengo la mizigo linalokarabatiwa kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye wakati alipofanya ziara katika Kiwanja hicho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...